Rio de la Plata

(Elekezwa kutoka Rio Plata)

Rio de la Plata (kihisp.: "mto wa fedha") ni mdomo wa pamoja wa mito ya Uruguay na Parana katika Amerika Kusini. Mito hii miwili inakutana takriban 290 km kabla ya kufikia pamoja katika bahari ya Atlantiki. Sehemu ya mwisho ya miendo yao ina umbo la kijazio kipana. Kutoka Atlantiki inaonekana kama hori ya bahari inayoingia ndani ya nchi na na kupokea mito hii miwili lakini inahesabiwa kuwa mto.

Río de la Plata kati ya Uruguay and Argentina
Rio de la Plata inavyoonekana kutoka angani; rangi ya kahawia inaonyesha maji ya mto Parana

Uruguay na Parana inapokutana ina upana wa 48 km; mwishoni ambako maji ya mto unafika baharini upana ni 220 km.

Jina la "Rio de la Plata" au "Mto wa Fedha" limetokana na historia ya kikoloni ambako fedha kutoka migodi ya Bolivia ilidafirishwa Ulaya kupitia njia hii ya maji.

Buenos Aires na Montevideo miji mikuu ya Argentina na Uruguay ambayo ni pia mabandari makuu ya nchi hizi iko pande mbili za mdomo wa mto.

Upande wa Montevideo maji yana kina cha kutosha kwa meli kubwa lakini bandari ya Buenos Aires inahitaji uchimbaji wa mara kwa mara kwa sababu upande wake maji si parefu sana.

Rio de la Plata ni mazingira ya pomboo aina ya "Franciscana" (au: "pomboo wa Rio Plata") ambaye ni pomboo wa mtoni wa pekee duniani ya kuingia baharini pia.

Viungo vya Nje

hariri
  Makala hii kuhusu maeneo ya Amerika Kusini bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Rio de la Plata kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.