Uruguay (mto)
Uruguay ni mto katika Amerika Kusini. Pamoja na mto Parana unaishia Rio de la Plata. Jina la Uruguay lamaanisha "mto wa ndege ya rangi nyingi".
Chanzo | milima ya Serra Geral (Brazil) |
Mdomo | Rio Plata |
Nchi | Brazil, Argentina, Uruguay |
Urefu | 1,790 km |
Kimo cha chanzo | takriban 1,800 m |
Mkondo | 4,622 m³/s |
Eneo la beseni | 370,000 km² |
Miji mikubwa kando lake | Concepción del Uruguay, Paysandu, |
Chanzo chake ni Brazil ya Kusini kwenye jimbo la Santa Catarina. Mwanzo wake ni mpaka kati ya majimbo ya Santa Catarina na Rio Grande do Sul ndani ya Brazil; baada ya mpaka kati ya Brazil na Argentina, halafu kati ya Argentina na Uruguay.
Jina la nchi ya Uruguay limetokana na mto huu. Asili ya jina la nchi ni "Jamhuri upande wa magharibi ya mto Uruguay".
Meli haziingii sana ndani ya Uruguay kutokana na maporomoko yake.
Viungo vya NjeEdit
- Salto Grande Hydroelectric System (Kihisp.)
- Trivia about Uruguay Archived Aprili 11, 2009 at the Wayback Machine. (Kihisp.)
- From Uruguay Blog about everything uruguayan (Kiing.)
Makala hii kuhusu maeneo ya Amerika Kusini bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Uruguay (mto) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |