Ripoti za Sheria ya Kenya

Ripoti za Sheria ya Kenya ni ripoti rasmi za sheria katika Jamhuri ya Kenya ambazo zinaweza kutajwa kesini katika mahakama ya Kenya (sehemu 21 ya Sheria). Hurejelewa hivi: [mwaka] KLR.

Ushauri wa uzinduzi wa Baraza la Taifa Sheria la ripoti za Sheria ulitokana na haja ya kuunganisha pengo kati ya kuripoti sheria na kushirikisha kuripoti sheria katika muundo wa serikali ya Kenya.

Baraza hilo liliundwa na kuzinduliwa rasmi tarehe 20 Mei 1996 chini ya Mhe. Bw Jaji Majid Cockar, na kisha Jaji mkuu. Baada ya uzinduzi huu, Baraza hili lilikuwa na mikutano kadhaa na kutayarisha bajeti lakini ilisitisha shughuli zake kutokana na ukosefu wa rasilimali.

Baraza hili halikuwa na uwezo wa kufanya kazi zake hadi mwanzoni wa mwaka wa 2001 wakati, chini ya uenyekiti wa Mhe Mr Jaji Bernard Chunga, kisha Jaji Mkuu, lilipatiwa makao, vifaa na wafanyakazi.

Ili kutimiza ahadi yake ya na maono, Baraza la Taifa la Ripoti za Sheria huwa na malengo yafuatayo:

  • Kuongeza kasi ya uchapishaji wa Ripoti za Sheria ya Kenya ili kuwa katika mwendo sawa na kalenda ya mahakama katika muda mfupi uwezekanavyo;
  • Kuchapisha ripoti ya awali na sasa katika mtindo wa kitabu fomu na pia katika mtandao kwa jina : www.kenyalaw.org;
  • Kushirikiana na serikali katika uchapishaji wa sheria za Kenya katika mtandao na nyenzo nyingine za kisheria;
  • Kuchapisha maoni ya kila mwezi na kila wiki juu ya masuala ya kisheria yanayoibukia kama katika maoni ya mahakama ;
  • Kuwakilisha katika Tume ya kuboresha sheria za Kenya katika maeneo ya sheria ambayo yana haja ya kuboreshwa;
  • Kusaidia umma, taasisi za elimu, mashirika yasiyo ya kiserikali na idara za serikali katika masuala yanayohusiana na sheria na habari nyingine za kisheria.

Masuala ya Baraza hili hutekelezwa kutoka ofisi ya karani sakafu ya chini katika mahakama ya kibiashara ya Milimani kando ya barabara ya Ngong katika eneo la Upper Hill (Community) katika Nairobi. Sehemu ya kwanza ya ripoti ya sheria ya Kenya ,[1981] KLR, ilitolewa tarehe 11 Januari 2002. Baraza hili limechapisha miaka 11 ya kitabu hiki (1981-1991) na wakati huo huo ripoti walichapisha ripoti ya sheria ya miaka minne (2001-2004).

Mwaka wa 2006, Barazahii ilianza uchapishaji wa taarifa maalumu ya sheria kuelezea masuala maalum katika sheria,kwa kuanzia na ripoti ya sheria ya Mazingira na Sheria Ardhi. Ripoti hizi huashiriwa hivi: KLR (E & L).

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu mambo ya sheria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ripoti za Sheria ya Kenya kama historia yake au uhusiano wake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.