Risala
Risala ni taarifa fupi inayosomwa mbele ya kiongozi mgeni rasmi kwa niaba ya kundi fulani la watu ili kutoa maelezo au kuonesha msimamo wa kundi hilo kwa kiongozi. Ni aina ya taarifa ambayo hupelekwa mtu au watu fulani inayoelezea haja inayotakiwa.
Risala hugawanyika katika sehemu kuu tatu, nazo ni:
- Mwanzo: Hapa panahusu sana salamu, ukaribisho na lengo la risala.
- Kati: ndiyo kiini cha risala ambacho huonesha mafanikio, matatizo, mapendekezo na kadhalika.
- Mwisho: wa risala hueleza msisitizo au shukrani.
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Risala kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |