Robert Holley
Robert William Holley (28 Januari 1922 – 11 Februari 1993) alikuwa mwanakemia kutoka nchi ya Marekani. Hasa alichunguza usanisi wa protini ndani ya mwili wa binadamu. Mwaka wa 1968, pamoja na Har Khorana na Marshall Nirenberg alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba.
Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Robert Holley kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |