Roketi
Roketi (Kiingereza rocket) ni chombo chenye umbo la bomba kinachopazwa angani kwa nguvu ya gesi inayotoka nje. Tofauti na injini ya jeti roketi hubeba fueli yote ndani yake kwa hiyo inafanya kazi pia katika ombwe pasipo na oksijeni au dutu nyingine inayohitajika kwa kuchoma fueli ndani ya injini yake.
Roketi hutumiwa kama silaha ya kijeshi, kama alama kiashiria katika hali ya dharura, fataki na kwa usafiri wa anga-nje.