Silaha ni kifaa cha mapigano dhidi ya wanadamu au wanyama.

Silaha za zama za mawe
Silaha ya karne ya 20

Inafaa kumtisha, kumwumiza au kumwua adui au kumletea hasara nyingine inayokusudiwa.

Kusudi la silaha ni matumizi

  • dhidi wanyama: uwindaji
  • dhidi ya watu: ama utetezi dhidi ya shambulio au shambulio lenyewe kwenye vita, jinai au fitina
  • ya kijamii: katika michezo (mashindano ya kufyatulia pinde au bunduki), kama sifa ya cheo au utamaduni

Katika historia watu wameweka nguvu nyingi katika maendeleo ya silaha. Kila sayansi na kila teknolojia huangaliwa na watu kwa faida yake katika utengenezaji wa silaha.

Silaha zimepatikana tangu zama za mawe. Upanga, pinde na mshale pamoja na mikuki zilikuwa silaha kwa milenia nyingi lakini ziliboreshwa tena na tena.

Tangu nyakati za kati silaha za moto zilianza kuenea duniani na kuboreka. Bunduki, mzinga na bombomu zilibadilisha uso wa vita. Karne ya 20 iliongeza vifaru na ndege za vita pamoja na viumbe vya sayansi ya kisasa kama silaha za nyuklia.