8°00′S 32°25′E / 8.000°S 32.417°E / -8.000; 32.417

Ziwa la Rukwa
Ziwa Rukwa
Ziwa Rukwa
Mahali Afrika ya Mashariki
Nchi zinazopakana Tanzania
Eneo la maji 800 - 3000 km² kutegemeana na kiasi cha mvua
Kina cha chini kuanzia 3.5 m
Mito inayoingia Songwe, Saisi
Mito inayotoka --
Kimo cha uso wa maji
juu ya UB
800 m
Miji mikubwa ufukoni --

Ziwa Rukwa ni ziwa kubwa la magadi nchini Tanzania. Liko upande wa kusini magharibi wa nchi, karibu na Zambia, kati ya Ziwa Tanganyika na Ziwa Nyasa.

Eneo la ziwa hubadilika mara kwa mara kufuatana na wingi wa mvua inayonyesha katika beseni yake.

Jiografia

hariri

Ziwa liko kwenye kimo cha mita 800 juu ya UB katika bonde ambalo ni mkono wa Bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki. Bonde hili ni sehemu ya kusini ya mkono wa magharibi wa bonde hili na mikono yote miwili inaungana huko Mbeya kabla ya kuendelea kwa pamoja katika Ziwa Nyasa.

Beseni ya ziwa line eneo la takriban 80,000 km². Urefu na upana wake hubadilikabadilika kulingana na kiasi cha mvua inayonyesha. Kati ya mito inayoingia ni mto wa Songwe pekee ulio na maji muda wote. Kuna taarifa ya kwamba ziwa lilipotea wakati mwingine isipokuwa beseni ndogo upande wa kusini Songwe inapoingia hubaki na maji. Kama maji ni mengi ziwa lina urefu wa kilomita 180.

Mazingira

hariri

Eneo la ziwa ni kavu sana na maji yake ni ya magadi. Kwa hiyo hakuna vijiji mbali na mito hasa upande wa kusini. Wakazi wa jirani ni hasa Wafipa, Wanyamwanga na Wasafwa.

Tanbihi

hariri


Viungo vya nje

hariri