SHARE in Africa ni shirika lisilo la kiserikali linalounga mkono elimu ya wasichana barani Afrika.[1]

Lilianzishwa na Shannon McNamara mnamo mwaka 2008 kwa lengo la kukabiliana na njaa ya vitabu barani Afrika kwa kuwapa wasichana vifaa vya kujifunzia.[2]

Tangu kuanzishwa kwake, SHARE imetoa fursa za elimu kwa maelfu ya wasichana nchini Tanzania. Hasa, wanafunzi 40,000 na walimu katika shule 9 barani Afrika wamepatiwa tani za vifaa vya kujifunzia ikiwemo vitabu 33,000, kompyuta ndogo na E-readers.[3] SHARE imejenga maktaba, kituo cha jamii, vyumba vya kompyuta na imeweka umeme na umeme wa jua katika shule za Tanzania.[4]

SHARE sasa imeweka juhudi zake katika kufadhili wasichana kwenda shule za sekondari.[5]

Shannon McNamara alizungumzia kazi ya SHARE ni kuelimisha wasichana katika Ikulu ya Marekani mnamo mwaka 2011 kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 100 ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake.[6] Pia aliandika blogi kwa Ikulu ya Marekani.

SHARE ina makao makuu St. Petersburg, Florida huko Marekani.

Marejeo hariri

  1. "Home Page | SHARE in Africa". www.shareinafrica.org. Iliwekwa mnamo 2019-04-04. 
  2. Restauri, Denise. "Teen Girl Wins Birth Lottery And Invests In The Future Of African Girls". Forbes (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2019-04-04. 
  3. "Home Page | SHARE in Africa". www.shareinafrica.org. Iliwekwa mnamo 2019-10-10. 
  4. Denise Restauri. "Why The Ripple Effect For Change Starts With Educating Girls", Forbes. (en) 
  5. [1]"Teen's Organization Helps Educate Girls in Tanzania". Wall Street Journal.
  6. "First Lady Praises SHARE at the White House". SHARE in Africa.