St. Petersburg, Florida
St. Petersburg ni jiji la pili kwa ukubwa katika eneo la Tampa Bay, baada ya Tampa. Pamoja na jimbo la Clearwater, majiji haya yanaunda jiji la Tampa–St. Petersburg–Clearwater Metropolitan, la pili kwa ukubwa katika Florida likiwa na idadi ya watu karibu milioni 2.8.
St. Petersburg iko kwenye pwani ya Pinellas kata ya Tampa Bay na Ghuba ya Mexico, na imeunganishwa na jimbo la Florida kuelekea kaskazini.
Historia
haririSt. Petersburg ilianzishwa mwaka 1888 na John C. Williams, ambaye alinunua ardhi, na kwa Peter Demens, ambaye alileta sekta ya reli katika eneo hilo. Kama sehemu ya mchezo wa kubashiri wa kutupa sarafu, mshindi, Peter Demens,akalipa jina eneo hilo baada ya mtakatifu Petersburg (Saint Petersburg) wa Urusi, wakati Williams alichagua kuiita hoteli ya kwanza kujengwa katika eneo hilo ambayo iliiwa hoteli ya Detroit, majina yote mawili yakiwa na majina ya miji yao ya kuzaliwa. St. Petersburg ilisajiliwa rasmi kama mji Februari 29,ya mwaka 1892 na kutambulika tena kama jiji mnamo 6 Juni 1903.
Makala hii kuhusu maeneo ya Marekani bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu St. Petersburg, Florida kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |