Sacrosidase
Sacrosidase, inayouzwa kwa jina la chapa Sucraid, ni dawa inayotumika kutibu upungufu wa kuzaliwa kwa enzaimu za sukrasi-isomalti (sucrase-isomaltase).[1] Matumizi yake yanaweza pia kusaidia utambuzi wa hali inayohusika.[1] Dawa hii inachukuliwa kwa njia ya mdomo kila wakati mtu anapokula.[1]
Madhara yake ya kawaida ni pamoja na maumivu ya tumbo, kichefuchefu, kuhara, shida ya kulala na maumivu ya kichwa.[1] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha athari za mzio.[1] Dawa hii inachukua nafasi ya kimeng'enya cha sukrasi (sucrase) ambacho husaidia katika uvunjaji wa sukari (sucrose) ili iwe katika aina rahisi zaidi.[1]
Sacrosidase iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 1998.[1] Nchini Marekani, dozi 118 ziligharimu takriban dola 8,700 za Marekani kufikia mwaka wa 2021.[2] Huko Ulaya ni dawa yatima.[3]
Marejeo
hariri- ↑ 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 1.6 "Sacrosidase Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 16 Julai 2017. Iliwekwa mnamo 9 Oktoba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Sucraid Prices, Coupons & Patient Assistance Programs". Drugs.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 9 Oktoba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Sacrosidase". SPS - Specialist Pharmacy Service. 31 Januari 2017. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 9 Oktoba 2021. Iliwekwa mnamo 9 Oktoba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Sacrosidase kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |