Sagittarius A*, kwa ufupi Sgr A* ni shimo jeusi katika kiini cha galaksi ya Njia nyeupe,[1][2][3] lenye tungamo wa takriban milioni 4.3 wa Jua.[4][5] Iko karibu na mpaka wa makundinyota ya Mshale na Nge, karibu 5.6° kusini mwa njia ya Jua,[6] karibu na Fungu la Kipepeo (M6)[7] na Shaula (λ Scorpii)[8].

Picha ya kwanza ya Sagitarius A* iliotolewa Mei, 2022.

Kitu hicho ni chenye kung'aa sana, na chanzo cha redio za angani na chenye mchanganyiko mkubwa wa mahala pamoja. Jina Sagittarius A* linafuata kutokana na sababu za kihistoria. Mwaka 1954[9] John D. Kraus, Hsien-Ching Ko, na Sean Matt waliorodhesha vyanzo vya redio walivyovitambulika kwa darubini ya redio ya Chuo Kikuu cha Ohio State[10] katika 250 MHz (mawimbi ya redio). Vyanzo hivyo vilipangwa na kundi la nyota na barua waliyopewa ilikuwa haielewwki, huku A ikiashiria chanzo cha redio angavu zaidi ndani ya kundi hilo. Asterisk ni kwa sababu ugunduzi wake ulichukuliwa kuwa "wa kusisimua"[11], sambamba na nomenclature kwa atomi za hali ya kusisimua ambazo zinaonyeshwa na asterisk (kwa mfano hali ya kusisimua ya Helium ingekuwa He*). Asterisk ilipewa (andikwa na_) na Robert L. Brown, mwaka 1982[12], ambaye alielewa kuwa uzalishaji mkubwa wa mawimbi redio kutoka katikati ya galaksi ulionekana ni kutokana na compact nonthermal radio object (kitu chenye mgandamizo mkubwa ya mawimbi redio).

Marejeo hariri

  1. Jeff Parsons (2018-10-31). "Scientists find proof a black hole is lurking at the centre of our galaxy". Metro (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-12-13. 
  2. "A 'mind-boggling' telescope observation has revealed the point of no return for our galaxy's monster black hole - The Middletown Press". web.archive.org. 2018-10-31. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-10-31. Iliwekwa mnamo 2022-12-13. 
  3. "Astronomers see material orbiting a black hole *right* at the edge of forever". SYFY Official Site (kwa en-US). 2018-11-07. Iliwekwa mnamo 2022-12-13. 
  4. Brooke Boen (2015-05-20). "Supermassive Black Hole Sagittarius A*". NASA. Iliwekwa mnamo 2022-12-13. 
  5. Revnivtsev, M. G.; Churazov, E. M.; Sazonov, S. Yu; Sunyaev, R. A.; Lutovinov, A. A.; Gilfanov, M. R.; Vikhlinin, A. A.; Shtykovsky, P. E.; Pavlinsky, M. N. (2004-10-01). "Hard X-ray view of the past activity of Sgr A in a natural Compton mirror". Astronomy & Astrophysics (kwa Kiingereza) 425 (3): L49–L52. ISSN 0004-6361. doi:10.1051/0004-6361:200400064. 
  6. Scott MacNeill. "Equatorial and Ecliptic Coordinates". Frosty Drew Observatory & Sky Theatre (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-12-13. 
  7. "Butterfly Cluster", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2022-12-09, iliwekwa mnamo 2022-12-13 
  8. "Lambda Scorpii", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2022-11-28, iliwekwa mnamo 2022-12-13 
  9. Kraus, J. D.; Ko, H. C.; Matt, S. (1954-12-01). "Galactic and localized source observations at 250 megacycles per second.". The Astronomical Journal 59: 439–443. ISSN 0004-6256. doi:10.1086/107059. 
  10. "Ohio State University", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2022-12-09, iliwekwa mnamo 2022-12-13 
  11. Goss, W. M.; Brown, Robert L.; Lo, K. Y. (2003-09). "The Discovery of Sgr A*". Astronomische Nachrichten (kwa Kiingereza) 324 (S1): 497–504. ISSN 0004-6337. doi:10.1002/asna.200385047.  Check date values in: |date= (help)
  12. "1982ApJ...262..110B Page 110". adsabs.harvard.edu. Iliwekwa mnamo 2022-12-13. 
  Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Sagittarius A* kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.