Salim Aziz
"Salim Aziz Salim" (16 Juni, 1989) ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Bakhresa Food Products Limited na Hotel Verde kutoka nchini Tanzania.[1] Ni afisa mdogo zaidi kwa Tanzania. Utendaji wake wa kazi ulianza katika divisheni ya juisi tangu 2010, akatoa matokeo yaliyopelekea kupanda cheo cha utendaji mkuu wa kampuni nzima ya Bakhresa Food inayojihusisha na vinywaji mbalimbali kama vile soda, maji, juisi na ice cream. Kitaaluma ni msimamizi wa biashara aliyopata shahada yake ya kwanza ya masomo ya biashara na usimamizi wa fedha kutoka Chuo Kikuu cha Salford, Uingerea.
Aidha, Salim Aziz ni mjumbe wa bodi ya Jumuiya ya Biashara ya Zanzibar (ZNCC ) Zanzibar, kwa kutegemea taaluma yake ya mamlaka ni mwakilishi wa Kamati ya Uchumi ya (ZNCC). Pia ni mmoja wa watu binafsi wa Jumuiya ya Marais Vijana (YPO).
Salim ni miongoni mwa vijana wanaong'ara ambao wana wadhifa mkubwa katika umri mdogo sana, anapendwa na vijana wengi wa Tanzania hasa wale aliowakukutana nao.[2][3] Amesaidia vijana wengi wa Kitanzania kufikia ndoto zao ikiwa ni elimu, programu za mafunzo, ajira, biashara kwa kuunda mifumo tofauti ya jukwaa kupitia nafasi yake katika kampuni.
Marejeo
hariri- ↑ https://www.linkedin.com/in/salim-aziz-bb172b32/?originalSubdomain=tz
- ↑ CEO wa BAKHRESA Ajitokeza HADHARANI, Atoa SIRI ya FAMILIA yake ILIVYOMSOMESHA, iliwekwa mnamo 2022-04-28
- ↑ SALIM AZIZ CEO BAKHRESA AKITOA SOMO KATIKA TUZO ZA ELIMU 2020, iliwekwa mnamo 2022-04-28