Sam Esmail
Sam Esmail (alizaliwa 17 Septemba, 1977) ni mwandishi, mtayarishaji na mwongozaji wa filamu, ambaye amejipatia jina kwenye tasnia ya filamu na televisheni.
Esmail ni Mmarekani mwenye asili ya Misri. Alisomea filamu katika Chuo Kikuu cha New York (NYU), ambapo alijikita katika uandishi wa filamu na televisheni. Baada ya kuhitimu, alianzia kwenye uandishi wa filamu na baadae kuhamia kwenye uongozaji na utayarishaji. Kipaji chake kilianza kung'aa alipounda mfululizo maarufu wa televisheni, Mr. Robot, ambao ulimkuza zaidi kwenye uwanja wa filamu na televisheni. Esmail amejitokeza kuwa mmoja wa waongozaji wa filamu wenye ushawishi mkubwa wa kizazi chake, akileta mtazamo wa kipekee kwenye hadithi na uwasilishaji. Kazi zake zimepokelewa vyema na wachambuzi na watazamaji, na kazi zake nyingi zimepokea tuzo na teuzi mbalimbali.
Maisha nje ya filamu
haririSam Esmail ni mpenzi wa teknolojia na mara nyingi ameonekana akidumbukizia teknolojia na ujanjaujanja wa kiteknolojia kwenye kazi zake. Uhusiano wake na Emmy Rossum, ambaye pia ni mugizaji mwenye jina kubwa, umemletea mafanikia kwenye kazi kazi zao zote. Wanaishi pamoja New York, na wamekuwa wakijitahidi kudumisha faragha yao licha ya umaarufu wao.
Baadhi ya kazi za Esmail
haririNa. | Kazi | Wasanii | Mwaka | Tuzo |
---|---|---|---|---|
1 | Mr. Robot | Rami Malek, Christian Slater, Carly Chaikin | 2015-2019 | Emmy, Golden Globe |
2 | Homecoming | Julia Roberts, Stephan James, Bobby Cannavale | 2018 | - |
3 | Comet | Justin Long, Emmy Rossum | 2014 | - |
4 | Briarpatch | Rosario Dawson, Jay R. Ferguson | 2020 | - |
5 | Metropolis | - | - | - |
6 | Angelyne | Emmy Rossum, Martin Freeman | 2022 | - |
7 | Gaslit | Julia Roberts, Sean Penn, Dan Stevens | 2022 | - |
8 | The Resort | William Jackson Harper, Cristin Milioti | 2022 | - |
9 | Leave the World Behind | Julia Roberts, Ethan Hawke, Mahershala Ali | 2024 | - |
10 | The American Throne | - | - | - |
Marejeo
hariri- https://www.imdb.com/name/nm2032864/ (Sam Esmail - IMDb)
- https://www.nytimes.com/2018/10/26/arts/television/sam-esmail-homecoming.html (The New York Times - Sam Esmail’s Vision for ‘Homecoming’)