Sean Bean
Shaun Mark Bean (amezaliwa 17 Aprili 1959) ni mwigizaji wa filamu na tamthilia kutoka nchini Uingereza. Bean amecheza vipindi kadhaa vya television na vilevile kuigiza sauti za katika gemu za kompyuta na matangazo ya television.
Sean Bean | |
---|---|
| |
Jina la kuzaliwa | Shaun Mark Bean |
Alizaliwa | 17 Aprili 1959,Sheffield, England |
Jina lingine | Sean Bean |
Kazi yake | Mwigizaji Mwigizaji wa sauti |
Ndoa | Debra James (m.1981) Melanie Hill (1990-1997) Abigail Cruttenden (1997-2000) Georgina Sutcliffe (2008-) |
Bean amecheza safu za juu kabisa katika filamu zilizonyingi, kuanzia ujangili hadi ushujaa. Sehemu yake ya kwanza kucheza na kujipatia umaarufu mkubwa ni baaada ya kucheza kama Richard Sharpe kutoka katika mfululizo wa kipindi cha televisheni maarufu kama Sharpe.
Tangu hapo akawa ameanza kufahamika kimataifa kwa kuigiza kama Boromir kutoka katika filamu ya The Lord of the Rings, Martin Septim katika filamu ya The Elder Scrolls IV: Oblivion video game, Alec Trevelyan kama mpinzani wa James Bond katika filamu ya Golden Eye, mshindani kubwa wa Nicolas Cage-Ian Howe katika filamu ya National Treasure, Gaidi Sean Miller kutoka katika filamu ya Harrison Ford-Patriot Games, Captain Rich kutoka katika filamu ya Flightplan akiwa na Jodie Foster, vilevile Odysseus kutoka katika filamu ya Troy.
Viungo vya nje
hariri- Sean Bean at the Internet Movie Database
- Sean Bean katika Yahoo! Movies
- Premiere Magazine: Sean Bean Interview Ilihifadhiwa 19 Septemba 2008 kwenye Wayback Machine.