Nchi isiyo na dini
(Elekezwa kutoka Serikali kutokuwa na dini maalumu)
Nchi zisizo na dini (yaani zisizo na dini rasmi) ni nchi zilizoamua kutosimama upande wa dini yoyote kati ya zile zinazofuatwa na wakazi wake.[1]
Nchi zisizo na dini rasmi Nchi zilizo na dini rasmi Utata au bila data |
Si kwamba nchi ya namna hiyo inapinga dini, bali inakusudia kuwatendea wakazi wote na miundo yao ya dini kwa usawa, bila upendeleo, ingawa pengine busara inadai kuzingatia wingi wa watu wanaozifuata, kwa mfano katika kukubali baadhi ya sikukuu katika kalenda ya taifa.
Kwa ajili hiyo siasa haitakiwi kutegemea dini yoyote, bali ustawi wa jamii unaolengwa kwa kuzingatia hoja ambazo nguvu yake inatokana na ukweli unaojulikana na akili tu.[2]
Tanbihi
hariri- ↑ Madeley, John T. S. and Zsolt Enyedi, Church and state in contemporary Europe: the chimera of neutrality, p. , 2003 Routledge
- ↑ http://www.allabouthistory.org/separation-of-church-and-state.htm
Marejeo
hariri- Temperman, Jeroen, State Religion Relationships and Human Rights Law: Towards a Right to Religiously Neutral Governance, BRILL, 2010, ISBN 9004181482
Makala hii kuhusu mambo ya siasa bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |