Dini (kutoka Kiarabu اﻟدﻴن, tamka: ad-din) inamaanisha jumla ya imani ya binadamu kadhaa pamoja na mafundisho wanayotoa kuhusu yale ambayo wanayazingatia ama kuyasadiki, yaani mambo ya roho, kama vile kuhusiana na Mungu, maisha na uumbaji.

Nembo za Kidini:
1.: Ukristo - Uyahudi - Uhindu - Nyota ya Baha'i
2.: Uislamu - Msalaba wa Kikelti - Falsafa ya China-Korea - Shinto
3.: Ubuddha - Usikhi - Ujaini - Ujaini
4.: Ayyavali - Upagani mpya - Msalaba wa chuma - Msalaba wa Kislavoni
Mganga wa kienyeji, Peru, 1988.

Ibada ni nguzo mojawapo iliyo dhahiri miongoni mwa dini kadhaa katika kuunganisha dhamira za mwenye kushika dini na mhimili wa imani, lakini dini inahusu pia mafundisho kuhusu maadili, mema na mabaya, imani na jinsi ya kushiriki katika jumuiya za waumini.

Kwa maana nyingine "dini" inataja jina kielelezo juu ya aina mbalimbali za imani jinsi inavyopatikana duniani, yaani jumuiya za kidini.

Dini kama jumuiya kubwa

 
Dini kuu na asilimia ya wafuasi kati ya watu wote duniani.

Dini kwa maana hiyo yenye wafuasi wengi duniani ni:

Pamoja na hizi kuna dini mbalimbali zinazojulikana tangu karne nyingi duniani hata kama idadi ya wafuasi si kubwa sana kwa mfano:

Pia kuna imani ambazo zinafanana kwa namna fulani, hivyo mara huhesabiwa kama imani mbalimbali za pekee, mara huhesabiwa kama kundi la dini zenye misingi ya pamoja au kama matawi ya imani moja. Zikitazamiwa pamoja idadi ya wafuasi ni kubwa kiasi lakini zikihesabiwa moja-moja idadi ya wafuasi si kubwa sana, kama vile:

Dini au Falsafa?

Hasa Asia ya Mashariki zimetokea mafundisho ambayo mara huhesabiwa kati ya dini mara kati ya falsafa. Mifano yake ni:

Wafuasi wao mara nyingine hufuata pia kwa wakati mmoja dini zingine kama vile Ubuddha au Ukristo.

Dini mpya

Historia inajua pia dini zilizotokea mara kwa mara katika nchi mbalimbali. Mfano wa dini iliyoanzishwa katika karne ya 19 na kusambaa kote duniani ni Baha'i. Kuna mifano mingi mingine. Si rahisi kuzitaja zote.

  • Kundi la "Scientology" ni mfano wa kundi dogo lililoangaliwa sana kwa sababu wafuasi kadhaa ni watu maarufu Marekani na Ulaya kutokana na filamu au magazeti.
  • Lakini miendo mipya yenye wafuasi wengi zaidi huko China (kama Falungong) haikuangaliwa ipasavyo kwa sababu wafuasi wake wako mbali zaidi na waandishi wa habari.
  • Rastafari ilianzishwa kama mwendo unaohesabiwa mara kama tawi la Ukristo, mara kama dini mpya kati ya wakazi wa Jamaika wenye asili ya Afrika tangu miaka ya 1930. Kupitia wapenzi wa muziki wa Jamaika imejulikana sana duniani. Jina na desturi zake kadhaa zimetumiwa kama mwendo wa kiutamaduni hata katika sehemu zingine za dunia ingawa idadi ya wafuasi wa dini hiyo ni ndogo.
  • Miendo ya kidini inayokua katika sehemu mbalimbali za dunia mara nyingi hazijulikani, hasa zikisambaa kati ya wasemaji wa lugha moja au katika sehemu fulani ya nchi moja tu. Mfano wake ni Dini ya Musambwa katika Kenya ya Magharibi tangu miaka ya 1940.

Zaidi ya hayo kuna miendo yenye tabia za kidini, ambayo hakuna makubaliano ya wataalamu kama ni dini au la, kwa mfano New Age na Yoga.

Dini kwa kipindi kirefu cha maisha ya mwanadamu imekuwa kitovu cha ustaarabu wa jamii husika. Hivyo kadiri jamii inavyobadilika ndivyo mambo mengi huongezwa ama kutolewa katika mapokeo yake ili hali kuakisi mazingira ya nyakati.

Katika wakati wa sasa, kumekuwepo kwa jitihada mbalimbali zinazopokea na kuchunguza misingi ya dini na maisha katika sura ya kisomi na hata kiudadisi.

Elimu ya Dini

 
Ramani ya uenezi wa dini duniani.

Kuna masomo mbalimbali ambayo huangalia na kuchunguza dini kwa kutumia mbinu za kitaaluma. Kati ya hizo kuna:

  • Teolojia ama tauhidi, ambayo ni matumizi ya mbinu za kiuanazuoni ndani ya dini fulani, kwa mfano teolojia ya Kiyahudi, ya Kikristo, ya Kiislamuu, n.k.
  • Falsafa ya dini inajaribu kutazama muundo wa fikra na mafundisho ya kidini. Inatumia mbinu na maswali ya falsafa ikitazama maswali kama: - je tunaweza kusema juu ya Mungu? - namna gani? - kuna maisha au uhai kupita kifo? - jinsi gani tunaweza kujua habari za mambo yajayo, uzima wa milele, asili na lengo la dunia?
  • Elimu ya dini inatazama dini mbalimbali na kuzilinganisha: jinsi zinavyobadilika, jinsi ibada zao zinaendelea, jinsi jumuiya zao zinakua au kupungua, nafasi ya dini katika maisha ya jamii n.k.
  • Takwimu ya dini ni somo linalojaribu kuhesabu idadi ya wafuasi wa dini mbalimbali.
  • Saikolojia ya dini inajaribu kuchunguza jinsi gani aina mbalimbali za imani zinahusiana na aina za roho za kibinadamu.
  • Ulinganisho wa dini unatazama hasa mafundisho na hali halisi ya dini mbalimbali jinsi zinavyofanana au kutofautiana: kwa mfano fundisho la Mungu mmoja katika Uyahudi-Ukristo-Uislamu-Uhindu; au fundisho la maono ya kiroho katika umistiki (Ukristo), kabbala (Uyahudi), usufi (Uislamu), tantra (Uhindi, Ubuddha).
  • Ukosoaji wa dini uko karibu na falsafa ya dini ukiwa na mwelekeo wa kuuliza maswali, kutamka wasiwasi, kuchunguza madai ya matamshi ya dini kulingana na misingi ya akili ya binadamu.

Marejeo

Ya awali
Ya baadaye
  • Barzilai, Gad; Law and Religion; The International Library of Essays in Law and Society; Ashgate (2007), ISBN 978-0-7546-2494-3
  • Borg, J. (1965), "The Serotonin System and Spiritual Experiences", American Journal of Psychiatry 160:1965-1969, November 2003
  • Brodd, Jefferey (2003). World Religions. Winona, MN: Saint Mary's Press. ISBN 978-0-88489-725-5.
  • Yves Coppens, Origines de l'homme - De la matière à la conscience, De Vive Voix, Paris, 2010
  • Yves Coppens, La preistoria dell'uomo, Jaka Book, Milano, 2011
  • Khanbaghi, A., The Fire, the Star and the Cross: Minority Religions in Medieval and Early Modern Iran (IB Tauris; 2006) 268 pages. Social, political and cultural history of religious minorities in Iran, c. 226-1722 AD.
  • King, Winston, Religion [First Edition]. In: Encyclopedia of Religion. Ed. Lindsay Jones. Vol. 11. 2nd ed. Detroit: Macmillan Reference USA, 2005. p7692-7701.
  • Korotayev, Andrey, World Religions and Social Evolution of the Old World Oikumene Civilizations: A Cross-cultural Perspective by , Lewiston, NY: Edwin Mellen Press, 2004, ISBN 0-7734-6310-0.
  • Palmer, Spencer J., et al. Religions of the World: a Latter-day Saint [Mormon] View. 2nd general ed., tev. and enl. Provo, Utah: Brigham Young University, 1997. xv, 294 p., ill. ISBN 0-8425-2350-2
  • Pals, Daniel L. (2006), Eight Theories of Religion, Oxford University Press
  • Ramsay, Michael, Abp. Beyond Religion? Cincinnati, Ohio: Forward Movement Publications, (cop. 1964).
  • Saler, Benson; "Conceptualizing Religion: Immanent Anthropologists, Transcendent Natives, and Unbounded Categories" (1990), ISBN 1-57181-219-9
  • Schuon, Frithjof. The Transcendent Unity of Religions, in series, Quest Books. 2nd Quest ... rev. ed. Wheaton, Ill.: Theosophical Publishing House, 1993, cop. 1984. xxxiv, 173 p. ISBN 0-8356-0587-6
  • Smith, Wilfred Cantwell (1962), The Meaning and End of Religion
  • Stausberg, Michael (2009), Contemporary Theories of religion, Routledge
  • Wallace, Anthony F. C. 1966. Religion: An Anthropological View. New York: Random House. (p. 62-66)
  • The World Almanac (annual), World Almanac Books, ISBN 0-88687-964-7.
  • The World Almanac (for numbers of adherents of various religions), 2005
  Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.