Shukria Barakzai (amezaliwa Kabul, Afghanistan, 1970) ni mwanasiasa, mwandishi wa habari na mwanaharakati wa ufeministi wa Kiislamu wa Afghanistan. Alikuwa balozi wa Afghanistan nchini Norway.[1] Pia ni mshindi wa Tuzo ya Mhariri wa Kimataifa wa Mwaka.

Picha ya Shukria Barakzai

Maisha ya Awali hariri

Barakzai alijiunga na Chuo Kikuu cha Kabul katika miaka ya 1990. Alilazimika kuacha masomo yake kutokana na ongezeko la vurugu kati ya serikali na Mujahideen. Mwezi wa Septemba 1996, Taliban waliiteka Kabul. Wakati huo, raia wengi, haswa tabaka la kati lenye elimu, walikuwa wameondoka kutokana na machafuko ya Taliban.


Wadhifa hariri

World Press Review, Worldpress.org ilitangaza Barakzai kuwa Mhariri wa Kimataifa wa Mwaka mnamo mwaka 2004.[2] Mnamo Desemba 2005, alitajwa Kuwa Mwanamke wa Mwaka na kipindi cha BBC Radio 4 Woman's Hour.[3]

Marejeo hariri

  1. "The Ambassador H.E. Ambassador Shukria Barakzai". Embassy of the Islamic Republic of Afghanistan, Oslo, Norway. 
  2. "International Editor of the Year Award". Worldpress.org. Iliwekwa mnamo 2016-09-26. 
  3. Wanawake wa Mwaka: Shukria Barakzai, BBC Radio 4.
  Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Shukria Barakzai kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.