Afghanistan
Afghanistan ( افغانستان, pia: Afuganistani) ni nchi ya bara la Asia. Inapakana na nchi za Pakistan, Uajemi, Turkmenistan, Usbekistan, Tajikistan na China.
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: hakuna | |||||
Wimbo wa taifa: Soroud-e-Melli | |||||
![]() | |||||
Mji mkuu | Kabul | ||||
Mji mkubwa nchini | Kabul | ||||
Lugha rasmi | KiPashto, KiFarsi | ||||
Serikali | Jamhuri ya Kiislamu Ashraf Ghani Abdullah Abdullah | ||||
Uhuru Tarehe |
Kutoka Uingereza 19 Agosti 1919 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
652,864 km² (41) N/A | ||||
Idadi ya watu - 2015 kadirio - 1979 sensa - Msongamano wa watu |
32,564,342 (40th) 13,051,358 43.5/km² (150th) | ||||
Fedha | Afghani (Af) (AFN )
| ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
(UTC+4:30) (UTC+4:30) | ||||
Intaneti TLD | .af | ||||
Kodi ya simu | +93
- |
Ni nchi ya milima mirefu mingi inayofunika 3/4 za uso wake. Kutokana na tabia ya nchi wakazi wengi huishi katika jumuiya za kikabila.
Jiografia
Afghanistan ni nchi bila pwani kwenye bahari yoyote. Sehemu kubwa ya eneo lake lenye km² 652,090 ni milima. Asilimia 90 za nchi iko mita 600 au zaidi juu ya UB ikiendelea kupanda hadi mita 7,485 kwenye ncha ya mlima Noshak. Safu za milima kubwa ni Hindu Kush na Pamir.
Katika kaskazini na kusini magharibi kuna maeneo ya tambarare yenye tabia ya jangwa. Maeneo makubwa ni yabisi na nusu jangwa au jangwa. Sehemu za milima zinapokea mvua na theluji, lakini mito mingi inayoanzia huko inapeleka maji yake nje ya nchi, kwenda Iran, Pakistan na Turkmenistan.
Hali ya hewa inategemea mahali na kimo. Sehemu za juu milimani huwa na jalidi kali wakati wa majira ya kipupwe na tambarare za chini huwa na joto kali wakati wa majira ya joto.
Mji | Halijoto ya mchana/usiku mwezi wa Januari | Halijoto ya mchana/usiku mwezi wa Julai |
---|---|---|
Herat | 9 °C/-3 °C | 37 °C/21 °C |
Kabul | 5 °C/-7 °C | 32 °C/15 °C |
Kandahar | 12 °C/0 °C | 40 °C/23 °C |
Historia
Afghanistan kama nchi ya pekee ilianza kutokea wakati wa karne ya 19. Kabla ya hapo nchi yote au sehemu mbalimbali zilikuwa sehemu ya milki jirani hata kama sehemu za eneo la Afghanistan zilijitegemea chini ya watawala wadogo. Kwa vipindi virefu vya historia Afghanistan ilikuwa sehemu ya milki za Uajemi (Iran).
Tangu miaka ya 1980 Afghanistan imekabiliwa na vita; mwaka 1979 Umoja wa Kisovyeti ulivamia nchi lakini ukapaswa kujiondoa tena mwaka 1989.
Vita vya wenyewe kwa wenyewe vilifuata kati ya vikundi vya wapinzani ambako nchi jirani ya Pakistan ilikuwa na athira kubwa kwa kutuma silaha na pesa.
Baada ya kipindi kifupi cha serikali ya kitaifa, kundi la Kiislamu la Taliban lilifaulu kuteka Kabul kwa msaada kutoka Saudia na Pakistan mwaka 1997.
Serikali ya Taliban ilikwisha kwa sababu walimruhusu Osama bin Laden pamoja na kundi lake la Al-Qaide kuwa na kimbilio nchini. Baada ya Shambulio la 11 Septemba 2001 Marekani ililipa kisasi kwa kushambulia Afghanistan.
Hali ya vita imeendelea ndani ya Afghanistan katika vita ya Marekani na NATO 2001-2014. Tangu Disemba 2014 nchi za NATO zilitangaza ya kwamba wamemaliza kuhudhuria katika mapigano na kuondoa sehemu kubwa ya wanajeshi kutoka Afghanistan. Vikosi vya NATO vimebakizwa shabaha ya kusaidia jeshi la kitaifa.
Watu
Mwaka 2015 wakazi walikadiriwa kuwa 32,564,342, wakiwemo wakimbizi milioni 2.5 wanaoishi Pakistan na Iran.
Kwa kuwa nchi iko kwenye njia zinazounganisha maeneo mbalimbali ya Asia, wakazi hao ni mchanganyiko mkuuː kabila kubwa ni la Wapashtuni (42%), halafu kuna Watajiki (27%), Wauzbeki (9%), Wahazara (8%) n.k.
Wengi wanaongea zaidi ya lugha moja (angalia orodha ya lugha za Afghanistan). Zile rasmi ni Kipashto (35%) na Kidari (50%), ambazo zote mbili ni za jamii ya Kiajemi kati ya Lugha za Kihindi-Kiulaya.
Upande wa dini, zaidi ya 99% ni Waislamu (90% Wasuni, 7% Washia n.k.). Ndiyo dini rasmi. Waliobaki ni Wazoroasta, Wakristo, Wahindu, Singasinga n.k.
Tazama pia
Kujisomea
- Vitabu
|
|
- Makala
- Meek, James. Worse than a Defeat. London Review of Books, Vol. 36, No. 24, December 2014, pages 3–10
Viungo vya nje
- Tovuti rasmi ya rais
- Afghanistan entry at The World Factbook
- Afghanistan katika Open Directory Project
- Wikimedia Atlas of Afghanistan
- Research Guide to Afghanistan
Nchi na maeneo ya Asia |
Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Uajemi | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani |
1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China. |
Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Afghanistan kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |