Sikusare otomnia

Sikusare otomnia [1] (ing. autumnal equinox) ni moja ya sikusare mbili za mwaka yaani siku ya usawa wa muda wa mchana na usiku katika maeneo mbali ya kanda ya ikweta.

Sikusare otomnia ni sikusare ambako kipindi cha mchana mrefu umekwisha na kipindi cha nusu mwaka kinaanza ambako usiku ni mrefu kuliko mchana. Kupunguka kwa muda wa mchana kunasababisha kuongezeka kwa hewa baridi hivyo katika nchi zenye majira baridi mimea huanza kuopoteza majani na kuandaa usingizi.

Sikusare ya otomnia inakadiriwa kuwa 21 Machi kwenye nusutufe ya kusini na 23 Septemba kwenye nusutufe ya kaskazini.

MarejeoEdit

  1. "otomnia" kutoka ing.-lat. "autumn / autumnus" ambayo ni kipindi kati ya majira ya joto na majira ya baridi kwenye nusutufe ya kaskazini ya dunia; matumizi ya KAST.