Silla
Silla (57 KK – 935 BK) (Tamka ɕilla) ilikuwa moja kati ya Falme Tatu za Korea, na moja kati ya nasaba iliokaa kwa muda mrefu sana katika historia ya Asia. Japokuwa ilianzishwa na Mfalme Park Hyeokgeose, ambaye anafahamika kama mwanzilishi wa famili ya Kikorea yenye jina la Park (박, 朴). Ukoo huu ulishikiria madaraka kwa takriban miaka yake 992 katika historia. Imeanza kama mtemi wa falme ndogo huko Samhan, pindi ilipoungana na China, Silla hatimaye ikaishinda falme mbili, Baekje mnamo 660 na Goguryeo mnamo 668. Baada ya hapo, ikawa Muungano wa Silla au Silla ya Baadaye, kama jinsi inavyotajwa mara nyingi kwa kuchukua sehemu ya Peninsula ya Korea, wakati sehemu ya kaskazini imeungana kama Balhae, nchi iliokuja kurithiwa na Goguryeo. Baada ya karibuni miaka 1000 ya utawala, Silla ikajivua kidogo na kuwa Falme Tatu za Baadaye, na kukabidhi mamlaka yake kwa mrithi wake wa nasaba ya Goryeo mnamo 935.[1]
Marejeo
hariri- ↑ http://www.shilla.or.kr/shilla_culture/ Ilihifadhiwa 21 Machi 2008 kwenye Wayback Machine. Retrieved on 2008-03-08
Viungo vya Nje
haririUfalme wa Korea Silla (Kabla-Muungano) |
|