Stella Obasanjo (14 Novemba 194523 Oktoba 2005) alikuwa mke wa rais wa Nigeria Olusegun Obasanjo kuanzia mwaka 1999 mpaka alipofariki, ingawa hakuwa mke wa rais mwaka 1976, wakati huo Obasanjo akiwa mkuu wa serikali wa kijeshi. Alifariki wakati anafanyiwa upasuaji wa kupunguza mafuta nje ya nchi.

Stella Obasanjo
Amekufa 23 Oktoba 2005
Nchi Nigeria
Kazi yake Mwanaharakati

Stella Obasanjo alikuwa mwanaharakati wa kisiasa, akiunga mkono juhudi kama women's liberation, youth as leaders of tomorrow, na the rehabilitation of a war-torn Nigeria.

Maisha ya awali na elimu

hariri

Obasanjo alitokea Iruekpen, Esan magharibi, Edo. Baba yake, Dr. Christopher Abebe, alikuwa kiongozi mkuu wa kampuni ya United Africa Company (UAC) ambaye alikuwa mwenyekiti wa kwanza mzaliwa wa Afrika wa kampuni hiyo ya UAC Nigeria.[1] Mama yake, Theresa, alihitimu katika chuo cha Pitman, London.[2]

Stella Abebe alianza elimu yake katika shule ya msingi iitwayo Our Lady of the Apostles Primary School. Kisha akajiunga na chuo cha St. Theresa, ambako alipata cheti cha elimu ya sekondari cha Afrika magharibi yaani West African School Certificate mwaka 1964 akipata daraja la kwanza. Miaka miwili baadaye alipata cheti cha elimu ya sekondari (kiin. High school). Akajiunga na chuo kikuu cha Ife, ambacho kwa sasa kinaitwa chuo kikuu cha obafemi Awolowo, kwa ajili ya shahada ya kwanza katika lugha ya Kiingereza, alihudhuria kuanzia mwaka 1967 mpaka 1969. Mnamo mwaka 1969 alihamia Uingereza kumalizia masomo yake, safari hii katika maswala ya bima , huko London na Edinburgh, Scotland, kuanzia 1970 mpaka 1974. [3]

Abebe alikamilisha elimu yake na cheti cha katibu wa siri kutoka chuo cha Pitman mwaka 1976. Alirejea Nigeria mwaka 1976.

Marejeo

hariri
  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Stella Obasanjo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.