Chuo Kikuu cha Strathmore

chuo kikuu cha kibinafsi nchini Kenya
(Elekezwa kutoka Strathmore University)

Chuo Kikuu cha Strathmore ni chuo cha binafsi mjini Nairobi, Kenya. Chuo cha Strathmore kilianzishwa mwaka wa 1961, kama chuo cha kiwango cha sita kinachofunza sayansi na sanaa za masomo, na kundi la wataalamu ambao walianzisha Hisani ya Kielimu inayoaminika sasa (Strathmore Educational Trust). Mtakatifu Josemaría Escrivá, mwanzilishi wa Opus Dei, aliwaongoza na kuwapa moyo kuanzisha chuo hicho hiyo.

Chuo kikuu cha strathmore
Chuo Kikuu cha Strathmore
Strathmore University
WitoUt omnes unum sint
Wito kwa KiswahiliThat all may be one
AinaPrivate
ChanselaMsg. Javier Echevarría, Prof. John Odhiambo (Vice Chancellor)
Walimu208
Staff422
Wanafunzi wa
shahada ya kwanza
5,088
Wanafunzi wa
uzamili
N/A
MahaliNairobi, Kenya
KampasiMadaraka (acre 40 (m2 162 000))
Tovutiwww.strathmore.edu

Mradi wa uhasibu umefanikiwa sana chuoni Strathmore :katika kipindi cha miaka kumi iliyopita, asilimia 60 ya wanafainali wa CPA nchini Kenya hutoka Strathmore.

Historia

hariri

Machi 1966, Wanafunzi 25 wa kwanza wa Uhasibu walijiunga na kidato cha sita, na kuanza kujiandaa kwa ajili ya mitihani ambo makao yake ni Uingereza (ACCA). Wanafunzi hawa walifadhiliwa na kampuni za Shell East Africa, British American Tobacco Kenya na East African Breweries.

Mnamo Oktoba 1982, Chuo kilianzisha kosi ya Uhasibu ya jioni na wanafunzi 60 walifadhiliwa na makampuni mbalimbali.

Mnamo Mwaka 1986, katika kuitikia ombi la Bodi ya Wadhamini, serikali ya Kenya ilihariji eka 5 ya ardhi iliyokatika barabara ya Ole Sangale, mtaa wa Madaraka. Muungano wa nchi za Ulaya na serikali ya Italia zilikubali kuiunga mkono mradi wa chuo kikuu huko Madaraka. Wahisani walitaka kuunga mkono chuo cha kielimu ambayo hutoa kosi katika Usimamizi na Uhasibu. Chuo cha Kianda, kijisehenu cha wakfu wa Kianda, ambacho kilikuwa na mipango ya maendeleo mapya wakati huo, kilikubali kuendesha kosi zao za kikazi katika chuo kikuu kipya ya Madaraka.

Ujenzi wa kampasi mpya ulianzia mwezi Septemba mwaka wa1989. Wakati huo huo, mnamo Januari 1991, Kituo cha Teknolojia ya Habari ulianzishwa katika kampasi ya Lavington kuendesha kozi za kompyuta ambayo ilipelekea utangulizi wa Taasisi kwa ajili ya Usimamizi wa Mfummo wa Habari ya shahada na shahada ya Juu. Mnamo Januari 1992, Kituo cha Mafunzo ya Mbali kilifunguliwa kutoa kosi ya Uhasibu kwa wanafunzi ambao hawawezi kuhudhuria mihadhara.

Mnamo Januari mwaka wa 1993, Chuo cha Strathmore kiliungana na kile cha Kianda na kuhamia katika barabara ya Ole Sangale iliyo katika mtaa wa Madaraka, jijini Nairobi. Mnamo Agosti 2002, Tume ya Elimu ya Juu iliituza Strathmore tuzo la barua ya mpito ya Mamlaka ya kufanya kazi kama Chuo Kikuu ikiwa na Kitivo cha Biashara na Kitivo cha mawasiliano na technologia.Mnammo Mwaka 2008, Strathmore ilipatiwa mkataba kuwa chuo kikuu kikamilifu. Strathmore imeanzisha skuli ya biashara ,iliyo na uhusiano na taaluma mbalimbali za juu za skuli ya Biashara, zikiwemo IESE na skuli ya Biashara ya Havard

Ofisi ya Strathmore waliopitia chuo hiki (SALO)

hariri

Ofisi ya waliopitia chuo hiki ni ofisi Mbegu ya kimataifa iliyoanzishwa nchini Kenya ikisaidiwa na wakfu wa Chuo Kikuu cha Strathmore (Strathmore University Foundation,Princeton, New Jersey, USA) ili kuendeleza na kusaidia mahusiano na shughuli baina ya Mbegu duniani kote. SALO anawajibu kwa kudumisha uhusiano wa Mbegu na Chuo Kikuu cha Strathmore.

Vitivo, Mashirika na Shule

hariri

Vitivo

hariri
  • Kitivo cha Biashara
  • Kitivo cha Teknolojia ya Habari
  • Kitivo cha Usimamizi wa Ukarimu

Mashirika

hariri
  • Institute of Humanities, Elimu na Mafunzo ya Maendeleo
  • Taasisi ya kuyaendeleza masomo
  • Taasisi ya mambo ya binadamu, Elimu na Mafunzo ya Maendeleo muda Desemba 2007 chini ya Kitivo cha Biashara.
  • Shule ya Uhasibu
  • Shule ya Utawala na Usimamizi
  • Shule ya Biashara ya Strathmore
  • Shule ya kuhitimu
  • Kituo cha Mafunzo ya Mbali
  • Kituo cha Strathmore cha Utafiti na Ushauri

Ushirika wa Kiakademia

hariri

Marejeo

hariri

Viungo vya nje

hariri