Sudusi ni sehemu ya sita ya jumla fulani. Neno limepokelewa katika Kiswahili kutoka Kiarabu ambako linaitwa سُدْس suds.

Katika familia ya Waislamu sudusi inataja sehemu ya urithi inayopokelewa na mama wa marehemu.

Mabaharia walitumia kifaa kinachoitwa Sudusi (ing. sextant) kwa kupima pembe za Jua na nyota baharini na hivyo wakiweza kukadiria mahali pao baharini.