Sufi
Sufi (kar. صوف suf[1]) ni jina kwa nyuzi laini kama pamba zinazotoka kwenye matunda ya msufi (miti ya jenasi Bombax, Ceiba na Rhodognaphalon).
Sufi hutumiwa kwa kujaza magodoro, kama kalafati kuziba nyufa kati ya mbao za mashua n.k. Haifai kwa kutengeneza nyuzi ndefu na vitambaa.
Mara nyingi neno hili linatumiwa pia kwa kutaja sufu yaani manyoya ya kondoo.