Sugar Ray Robinson
Sugar Ray Robinson (alizaliwa akiitwa Walker Smith Jr., 3 Mei 1921 - 12 Aprili 1989) alikuwa bondia kutoka Marekani. Alishinda ubingwa wa ulimwengu wa uzito wa welter na uzani wa kati.
Baadhi ya wanahistoria wa mchezo wa ngumi wamemtaja kama bondia bora aliyewahi kuishi.
Maisha ya awali
haririRobinson alizaliwa huko Ailey, Georgia akiwa mdogo wa watoto watatu. Babake alikuwa mkulima aliyehamia baadaye Detroit, mji mkubwa katika kaskazini ya Amrekani, alipopata kazi ya ujenzi.
Baada ya kutengana kwa wazazi, Robinson pamoja na mamake alihamia Harlem, New York akiwa na umri wa miaka 12. Kiasili alikuwa na ndoto ya kuwa daktari lakini baada ya kupata matatizo shuleni, aliamua kuingia katika mchezo wa ngumi. Alikuwa bado mdogo hivyo alitumia hati ya kuzaliwa ya rafiki yake Ray Robinson akaendelea kutumia jina lake[1].
Bondia
haririWakati wa kuwa bondia wa ridhaa hakudhindwa hata mara moja. Tangu 1940 alikuwa bondia wa kulipwa akashinda taji la uzito wa welter kutoka kwa Johnny Bratton mnamo 1946. Kisha akamshinda Jake LaMotta kwa ubingwa wa uzani wa kati mnamo 1951. Alipoteza na kupata tena cheo kutoka kwa Randy Turpin kabla ya kujaribu, na kushindwa na Joey Maxim kwa ubingwa wa uzani wa uzito mdogo mnamo 1952. Alistaafu baadaye mwaka huo. Aliamua kurudi tena akashinda taji la uzani wa kati tena mnamo 1955. 1957 alishindwa na Gene Fullmer lakini alirudia kumshinda katika mchezo wa marudiano. Baadaye mwaka uleule, Carmen Basilio alimshinda Robinson kwa taji lile, lakini Robinson alirudi kumshinda mnamo 1958 ili kupata ubingwa tena.
Kifo
haririRobinson aliendelea kupigana hadi miaka ya 1960. Alikufa kwa ugonjwa wa kisukari na ugonjwa wa Alzheimer akiwa na umri wa miaka 67 huko Culver City, California mnamo 1989.
Viungo vya nje
hariri- Boxing record Ilihifadhiwa 20 Aprili 2006 kwenye Wayback Machine.
- The Official Site of Sugar Ray Robinson Ilihifadhiwa 4 Novemba 2008 kwenye Wayback Machine.
Alitanguliwa na Marty Servo Vacated |
World Welterweight Champion 20 Dec 1946 – 14 Feb 1951 Vacated |
Akafuatiwa na Johnny Bratton |
Alitanguliwa na Jake LaMotta |
World Middleweight Champion 14 Feb 1951 – 10 Jul 1951 |
Akafuatiwa na Randy Turpin |
Alitanguliwa na Randy Turpin |
World Middleweight Champion 12 Sep 1951 – Dec 1952 Retired |
Akafuatiwa na Carl (Bobo) Olson |
Alitanguliwa na Carl (Bobo) Olson |
World Middleweight Champion 9 Dec 1955 – 2 Jan 1957 |
Akafuatiwa na Gene Fullmer |
Alitanguliwa na Gene Fullmer |
World Middleweight Champion 1 May 1957 – 23 Sep 1957 |
Akafuatiwa na Carmen Basilio |
Alitanguliwa na Carmen Basilio |
World Middleweight Champion 25 Mar 1958 – 22 Jan 1960 |
Akafuatiwa na Paul Pender |