Sumu ya methanoli
Sumu ya methanoli ni sumu kutoka kwa methanoli.[1] Dalili zake zinaweza kujumuisha kupungua kwa kiwango cha ufahamu, uratibu duni, kutapika, maumivu ya tumbo na harufu maalumu kwenye pumzi.[1][2] Kupungua kwa uwezo wa kuona kunaweza kuanza mapema kama saa kumi na mbili baada ya kuambukizwa.[2] Matokeo ya muda mrefu yanaweza kujumuisha upofu na kushindwa kwa figo.[1] Sumu na kifo vinaweza kutokea hata baada ya kunywa kiasi kidogo.[1]
Sumu ya methanoli | |
---|---|
Mwainisho na taarifa za nje | |
Kundi Maalumu | Dawa ya dharura |
Dalili | Kupungua kwa kiwango cha ufahamu, uratibu duni, kutapika, maumivu ya tumbo, harufu maalumu kwenye pumzi[1][2] |
Visababishi | Methanoli (kama vile kupatikana katika kiowevu cha kuosha kioo)[1][2] |
Njia ya kuitambua hali hii | Asidi ya damu acidosis, kuongezeka pengo la osmol, kiwango cha methanoli ya damu[1][2] |
Utambuzi tofauti | Maambukizi, kuathiriwa na pombe yenye sumu, ugonjwa wa serotonini, ketoacidosis ya kisukari[2] |
Matibabu | Dawa ya kupambana na sumu, kuondoa sumu na vitu vingine vyenye madhara kutoka kwa damu[2] |
Dawa | Fomepizole, ethanol[2] |
Utabiri wa kutokea kwake | Nzuri kwa matibabu mapema[1] |
Idadi ya utokeaji wake | Matumkio 1,700 kwa mwaka (Marekani)[3] |
Sumu hii mara nyingi hutokea kufuatia unywaji wa kioevu cha kuosha kioo.[2] Hii inaweza kuwa kwa bahati mbaya au kufanywa kwa makusudi katika jaribio la kufa kwa kujiua.[1] Sumu hii pia inaweza kutokea kwa nadra sana kupitia mfiduo mkubwa wa ngozi au kupumua moshi.[1] Methanoli inapovunjwa na mwili husababisha formaldehyde, asidi ya formic na formate ambayo husababisha sumu nyingi.[2] Utambuzi wake unaweza kushukiwa wakati kuna asidi au kuongezeka kwa pengo la osmol na kuthibitishwa kwa kupima moja kwa moja viwango vya damu.[1][2] Hali nyingine zinazoweza kutoa dalili zinazofanana ni pamoja na maambukizi, kuathiriwa na alkoholi nyingine zenye sumu, ugonjwa wa serotonini, na ketoacidosis ya kisukari.[2]
Matibabu ya mapema huongeza uwezekano wa matokeo mazuri.[2] Matibabu yake ni pamoja na kuleta utulivu wa mtu aliyeathiriwa, ikifuatiwa na matumizi ya dawa ya kupambana na sumu (antidote).[2] Dawa inayopendekezwa ni fomepizole, ambapo ethanol pia inaweza kutumiwa ikiwa hii haipatikani.[2] Hemodialysis pia inaweza kutumika kwa wale ambapo kuna uharibifu wa kiungo au kiwango cha juu cha asidi.[2] Matibabu mengine yanaweza kujumuisha sodium bicarbonate, folate, na thiamine.[2]
Milipuko imetokea kutokana na uchafuzi wa pombe ya kunywa.[2] Hii ni kawaida zaidi katika ulimwengu unaoendelea.[2] Katika mwaka wa 2013, zaidi ya kesi 1700 zilitokea Marekani.[3] Wale walioathirika kwa kawaida ni watu wazima na wanaume.[3] Sumu hii ya methanoli imeelezewa mapema kama mwaka wa 1856.[4]
Marejeo
hariri- ↑ 1.00 1.01 1.02 1.03 1.04 1.05 1.06 1.07 1.08 1.09 1.10 Kruse, JA (Oktoba 2012). "Methanol and ethylene glycol intoxication". Critical Care Clinics. 28 (4): 661–711. doi:10.1016/j.ccc.2012.07.002. PMID 22998995.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 2.00 2.01 2.02 2.03 2.04 2.05 2.06 2.07 2.08 2.09 2.10 2.11 2.12 2.13 2.14 2.15 2.16 2.17 2.18 Beauchamp, GA; Valento, M (Septemba 2016). "Toxic Alcohol Ingestion: Prompt Recognition And Management In The Emergency Department". Emergency Medicine Practice. 18 (9): 1–20. PMID 27538060.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 3.0 3.1 3.2 Ferri, Fred F. (2016). Ferri's Clinical Advisor 2017: 5 Books in 1 (kwa Kiingereza). Elsevier Health Sciences. uk. 794. ISBN 9780323448383. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-09-08.
- ↑ Clary, John J. (2013). The Toxicology of Methanol (kwa Kiingereza). John Wiley & Sons. uk. 3.4.1. ISBN 9781118353103. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-09-08.