TV janja (kwa Kiingereza: Smart Tv) ni runinga ambayo imeunganishwa na mitandao hivi kwamba yaweza kumburudisha mtazamaji kwa kuona video zilizoko kwa wavuti wa Netflix, Amazon Prime, Hulu na nyinginezo. Hii huwa tofauti na runinga ya kidijiti ambayo huweza tu kuunganishwa na vyombo kama HDMI, AV na USB. Tv janja basi inaipiku runinga dijitali kwani yaweza kutembelea mitandao na kuungana na HDMI, USB na AV.

TV janja pia hudhibitiwa na mfumo kama vile wa Web Os au Android Ilihifadhiwa 3 Septemba 2021 kwenye Wayback Machine.. Kampuni zinazotengeneza tv janja huweka mifumo yao kwa runinga hizo. Kwa mfano kampuni za LG na Samsung zimeweka mifumo yao kwa tv janja ambazo wametengeneza. Katika mifumo hiyo, mtazamaji anaweza kupakua programu zinginezo na pia kutazama vindeo zilizoko kwa mitandao ya Youtube, Netflix na Amazon Prime.

Vipengele vilivyo kwa TV janja

hariri

Tv janja pia huweza kudhibitiwa kwa kutumia sauti tu ya mtazamaji bila kutumia remote control. Ili kufanya hivi, huwa zimewekwa programu kama voice recognition, Alexa na Google Assistant.

Kipengele kingine cha tv janja ni kuwa huenda zikatumika kama tarakilisha ya kawaida katika kutembelea wavuti mbalimbali. Mtumiaji huenda akatumia remote control kufanya hivi au sauti yake kama runinga yake inaweza kutumia voice recognition.

Matumizi ya TV janja

hariri

Tv janja huweza kutumika kwa njia zifuatazo:

  1. Kwa mitandao ya kijamii-- Mtumizi huenda akatumia tv janja yake katika kutembelea wavuti za mitandao ya kijamii (social networks)
  2. Kuweka matangazo

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.