Tafsida ni tamathali za semi ambazo ni za adabu na huwa zinatumika kupunguza ukali wa maneno.

Neno tafsida lina kisawe tauria. Ni mojawapo ya tamathali za semi. Ni utumiaji wa lugha ya adabu na heshima ili kuondoa ukali, matusi au fedheha na lugha tovu kiadabu. Tafsida hutumika hususan katika mazungumzo na hata katika fasihi andishi kama vile riwaya, tamthilia na ushairi.

Mifano:

  • Badala ya kusema "Mama yule ana mimba." Sema "Mama yule ni mjamzito."
  • Badala ya kusema "Mama anakaribia kuzaa mtoto." Sema "Mama anakaribia kujifungua mtoto."
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Tafsida kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.