Tagged.com ni mfumo wa mtandao[1] wa kijamii ulioanzishwa mnamo 2004. Tagged ni mojawapo ya mitandao inayozua malalamiko kutoka kwa wateja kwa kupokea barua pepe za uwongo[5] na unachukuliwa kama mtandao wa kuwadanganya watu na barua pepe wasizozihitaji” na “zisizokuwa za maana" na watetezi wa wateja dhidi ya ulaghai.[7][9][10] Afisi kuu iko San Francisco, Kalifonia, Marekani.[2]

Tagged
Aina ya shirikaSocial networking site
Pahali pa makao makuuSan Francisco, California, United States
MmilikiTagged Inc.
Tovutihttp://www.tagged.com
KusajiliRequired
Tarehe ya uzinduziOktoba 2004
Hali ya sasaActive

Historia

hariri

Tagged Inc. ni mtandao ulioanzishwa na wanafunzi waliohitimu wa Chuo kikuu cha Harvard wajasirimali Greg Tseng na Johann Schleier-Smith".[3] Wawili hao walikuwa wameanzisha Avavin, Inc., ambayo ilikuwa ni kampuni ya kulinganisha vitabu.[14] Tseng hapo awali alikuwa mwanzilishi na Mkurugenzi Mkuu wa mtandao huru wa 'Jumpstart Technologies', [4] ambao baadaye ulitozwa faini ya $ 900.000 kwa madai ya ukiukaji wa sheria za CAN-spam, ambayo ilikuwa ndiyo adhabu kubwa iliyowahi kupeanwa ya kosa la aina hiyo. [5] Tseng amehitimu na A.B. katika kemia, fizikia na hisabati kutoka Chuo Kikuu cha Harvard. Schleier-Smith pia amehitimu na A.B. katika fizikia na hisabati kutoka Chuo Kikuu cha Harvard. [onesha uthibitisho]


Mtandao huu wa Tagged ambao mwanzoni iliwalenga vijana wa US, ulifunguliwa kwa watumiaji duniani kote wenye umri wa miaka 13, mnamo Oktoba 2006 na bado unaendelea kudumisha usalama mkali kwa watumiaji walio chini ya miaka 18. [6] Watumiaji walio juu ya umri wa miaka 16 na umma hawawezi kuona habari za kibinafsi za watumiaji walio na umri wa miaka 13 na 14, na habari za kibinafsi za watumiaji wa miaka 15-16 huwa zimefichwa ili zisisomwe na umma na watumiaji wa zaidi ya miaka 18. Njia pekee ya kuongeza vijana kama marafiki ni kwa kujua au barua pepe au majina ya kifamilia kuomba urafiki na mtumiaji mdogo ni lazima akubali ombi hilo la urafiki. Hata hivyo, hatua hizi za usalama hazina mafanikio kamili. Katika mwezi wa Februari 2009 mwalimu wa shule ya upili alikamatwa baada ya kuwa na uhusiano wa kimapenzi na msichana mwenye umri wa miaka 14 aliyekutana naye kwenye tagged.com. Mwalimu huyo mwenye umri wa miaka 32 alikuwa na marafiki wa kike zaidi ya 100 waliokuwa wa umri chini ya miaka 17. [7]

Mnamo Machi 2008 shirika la Microsoft lilitangaza makubaliano ya ushirika wa kibiashara na mtandao wa Tagged, Facebook, Linkedln, Bebo na hi5 kuhusu anwani za barua pepe APIs[8][9] makubaliano hayo yametekelezwa.[10] Ushirikiano mwingine unajumuisha Slide, RockYou, PhotoBucket, Meebo,[11] Razz[12] na Jangl.[13]

Tagged ina wafanyakazi 40 kwa sasa. [14] Tagged ni mwanachama wa Social Media Advertising Consortium, ambao ni muungano wa sekta ya biashara unaolenga kuongeza ushiriki na viwango ndani ya chama. [15]

Mnamo Septemba 2009, Hitwise iliripoti kuwa Tagged.com ilikuwa katika nafasi ya tatu katika ukubwa baina ya mitando ya jamii nchini Marekani kulingana na watu wanaoutumia kila mwezi.[16]

Mtandao

hariri

Baada ya kusainiwa ili kufungua akaunti ya bure, watumiaji wa Tagged wanaweza kurekebisha ukurasa wa habari zao za kibinafsi, ambapo watumiaji wanaweza kupakia picha na albamu, kupokea na kukubali ujumbe kutoka kwa watumiaji wengine, kutia wasifu wao na habari kuhusu yale wanayoyapenda, kutumiana "pepeso" za kirafiki , na kuweka fahamisho za jinsi wanavyoendelea ili kuwajulisha marafiki zao walipo na matendo yao. Watumiaji wanaweza kuona watumiaji wengine ambao wamezisoma habari zao hivi karibuni, kutuma vishikizo vya kirafiki kwa marafiki zao, na ainisha video kulingana na zile zilizotazamwa na wengi, zilizopewa nafasi za juu na zilizopendwa na wengi. Watumiaji wanaweza kutuma zawadi za kirafiki kwa marafiki zao. Zawadi hununuliwa kwa "dhahabu" ambazo watumiaji wanaweza kununua kwa fedha halisi (tovuti inaruhusu ununue kupitia PayPal, pesa taslimu, malipo ya Amazon au kwa simu) au kwa kukamilisha ahadi au kazi maalum. Kuna vijumba vya kupiga gumzo vinavyoonekana ambavyo watumiaji huhusika katika muda halisi wa kuzungumza katika mtandao katika "vyumba" tofauti kulingana na umri wao na mihemko yao. Mtandao wa Tagged ambao una mwelekeo wa uhusiano na kupendana, huwa unaruhusu watumiaji kutuma na kupokea jumbe za "Luv", "Winks" na "Meet Me", injini ya upimaji ambayo inaruhusu watumiaji kupima uzuri wa picha zilizowekwa kwa hiari na wengine. Michezo ya video ya mtandao inayopatikana kwenye tovuti hii ni pamoja na michezo ya Zynga kama vile "Poker", "Pets", ambapo watumiaji wanaweza kupata fedha kwa kununua watu kama kipenzi, na "Mafia Wars". Tarehe 30 Oktoba 2009, Tagged ilitangaza kuwa walikuwa wanaanzisha mchakato mpya rahisi wa kujiunga. [17]

Ubishani

hariri

Makala katika Jarida la Time yaliita Tagged "Matandao unaoudhi mno duniani".[31] Tagged huuliza anayetumia anwani ya barua pepe na kitambulisho chake na pia neno la siri, huangalia anwani za barua pepe za watu na kutuma mwaliko kwa kurudia kwa watu wasiotumia mtandao huu wa Tagged, kwa kuanzia kwa kujulisha kuwa wameongezwa kuwa rafiki au wamealikwa kutazama picha kwa Tagged. Njia hii imesababisha kushutumiwa kwa teknolojia ya habari na watumizi. Barua pepe hizi zilijadiliwa na Black Web 2.0.[18] Hali hii ya jumbe hizi kufanana na virusi imetajwa sana, ikiwa ni pamoja na urban legend site Snopes.com. Gazeti la New York Times lilirejelea mazoea haya kama ufutaji wa majina".[19]

Mnamo Julai 2009 Mkuu wa sheria wa New York Andrew Cuomo alitangaza azimio lake la kushtaki Tagged.com kwa "kutumia barua pepe za uongo katika biashara na kuingilia faragha".[38] Kulingana na habari zilizotolea na vyombo vya habari, Tagged.com ilijihusisha na "barua pepe za udanganyifu, wizi wa vitambulisho, na kuingilia faragha". Tagged.com iliafikiana na Mkuu wa sheria wa New York ambapo walikubaliana Tagged.com wangelipa dola milioni 500,000 na kurekebisha mbinu zao za uuzaji kwenye mtandao.[39]

Wakati uo huo, Tagged.com walikubaliana na Jimbo la Texas kuhusu maswala ya sheria. Katika makubaliano, Tagged.com ilikubali kulipa dola 250,000 kama ada ya adhabu. Masharti mengine yalikuwa kufichua kwa njia “dhahiri na wazi” habari za watumizi katika anwani za barua pepe, ikitoa, kwa mtumiaji, njia mwafaka ya kuepuka hatua hiyo na kumwonyesha barua pepe maalum atakazotumiwa.[40]

Kutoka Febuari 2009 Tagged.com imezuiliwa nchini Qatar na ISP, Qtel, baada ya malalamiko kadhaa kutoka kwa umma.[41] Tagged.com ulikuwa mojawapo ya mitandao kumi iliyotumika sana nchini Qatar.[20]

Demografia ya watumizi

hariri

Mtandao huu wa Tagged ambao mwanzoni ulilenga vijana pekee, sasa hivi una wanachama wengi kutoka katika kikundi cha umri wa miaka 35-49 kuliko kikundi chochote kingine. [21] Idadi ya vijana walio wanachama katika Marekani sasa ni 8% tu. [21] Kila mwezi, Tagged hutembelewa na watumiaji milioni 7.6 kutoka US kila mwezi na watumiaji milioni 26 duniani kote. [21] Asilimia sabini na tano ya watumiaji huwa na pato la chini ya $ 60,000 kila mwaka na 61% huwa na elimu isiyofikia chuo cha taasisi. [21]

Marejeo

hariri
  1. "Social Networking Growth". cbronline.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-01-04. Iliwekwa mnamo 2009-06-09.
  2. [11] ^ "Internships." Tagged. Retrieved on 11 Juni 2009.
  3. "Who Says Money Can't Buy Hipness?". BusinessWeek. Iliwekwa mnamo 2009-11-23. {{cite web}}: Italic or bold markup not allowed in: |publisher= (help)
  4. 15] ^ Greg Tseng's speaker bio at the Authentication and Online Trust Summit 2007
  5. [16] ^ "FTC Slams Spammer in Pocketbook." Ilihifadhiwa 12 Aprili 2011 kwenye Wayback Machine. Tume ya Shirikisha ya Biashara. 23 Machi 2006. Retrieved on 11 Juni 2009.
  6. http://www.techcrunch.com/2007/05/09/tagged-turns-profitable-may-be-fastest-growing-social-network/
  7. [19] ^ http://www.gilroydispatch.com/news/254074-high-school-math-teacher-arrested-for-sex-crimes-with-14-year-old Ilihifadhiwa 2 Juni 2009 kwenye Wayback Machine. High school teacher math arrested for sex crimes with 14-year-old
  8. Windows Live Dev Blog
  9. techcrunch
  10. techcrunch
  11. techcrunch
  12. [24] ^ Raz press release Ilihifadhiwa 21 Januari 2016 kwenye Wayback Machine.
  13. [25] ^ East Bay Business Times
  14. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-01-31. Iliwekwa mnamo 2009-12-07.
  15. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-04-22. Iliwekwa mnamo 2009-12-07.
  16. "Experian Hitwise : Facebook Visits Increased 194 Percent in Past Year". Hitwise. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-11-03. Iliwekwa mnamo 2009-11-26.
  17. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-08-14. Iliwekwa mnamo 2009-12-07.
  18. Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref> tag; no text was provided for refs named Did You Get Tagged Yet
  19. Typing an E-Mail Adress, na Giving Up Your Friends as Well
  20. [42] ^ "Complains forced Qtel to block top-rated site." Ilihifadhiwa 5 Julai 2009 kwenye Wayback Machine. The Peninsula at Gulf Base. 9 Februari 2009. Retrieved on 11 Juni 2009.
  21. 21.0 21.1 21.2 21.3 "tagged.com - Quantcast Audience Profile". Quantcast. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-07-18. Iliwekwa mnamo 2009-11-24.

Viungo vya nje

hariri