Tamy Moyo

Mwigizaji na mwanamuziki wa Zimbabwe

Thamsanqa 'Tamy' Moyo (alizaliwa Harare, Zimbabwe, Januari 1998) ni mwigizaji wa kike na mwimbaji wa Zimbabwe.[1] Anajulikana Sana kwa wimbo wake wa Ndibereke aliouimba mwaka 2016, mwaka 2020 Alipata jukumu la kuigiza katika filamu ya Gonarezhou.[2]

Maisha binafsi hariri

Baba yake, Richard Kohola ni mtangazaji wa Star FM Zimbabwe maarufu kwa jina la ‘’RK The Music Doctor’’. Alilelewa na mama yake Doris Moyo Pamoja na babu yake Makwara.[3]

Kazi hariri

Akiwa na miaka 7 pekee, alianza kuimba katika kwaya ya watu wazima. Alihitimu elimu yake ya msingi kutoka shule ya Lusitania na baadae kuendelea na masomo ya sekondari katika shule ya Westridge High School. Alipofika kidato cha kwanza, wakati huo akiwa na miaka 13, alijiunga na wanamuziki mashuhuri kama Joe Thomas, Oliver Mtukudzi, Stunner, Ba Shupi, na Alexio Kawara. Baadaye akawa balozi wa Watoto nchini Zimbabwe, na kufanikiwa kuwa balozi mdogo zaidi katika historia ya Zimbabwe. Mnamo mwaka 2008, Tamy aliunda kikundi cha kwaya kwa jina la Uganda African Choir, akiwa na wengine watatu, hii ilikua huko Madison Square, New York wakati wa shughuli ya kihisani.[1][3]

Aliandika na kuimba wimbo kwa jina la, Cry For Help, wimbo huo ulihamasisha Watoto kupiga simu za kuomba msaada wakiwa na shida kwenda namba 116 bure. Mnamo mwaka 2012, kwa mara ya kwanza Tamy aliachia albamu yake ya kwa jina la Celebrate Yo Lyf.[3] hii ilimfanya apate nafasi ya kutumbuiza katika matamasha makubwa ya muziki nchini Zimbabwe kama ‘’Harare International Festival of the Arts’’ na Shoko Festival. Pia alishiriki katika sherehe za tuzo za ‘’National Arts Merit Awards’’ na mashindano ya ulimbwende ya ‘’Miss Tourism Zimbabwe’’ ambamo alitumbuiza mwezi Novemba mwaka 2016.[1]

Mwaka 2017, Tamy alialikwa na mtayarishaji wa filamu Sydney Taivavashe kuwa mhusika katika filamu ya Gonarezhou. Filamu hiyo ilitengenezwa kwa ushirikiano na Shirika la wanyamapori na uhifadhi wa Wanyama la nchini Zimbabwe.[4] In the film Tamy played the role 'Chipo' as his debut cinema appearance.[5] In the same year, she had her first nomination in the National Arts Merit Awards (NAMA awards) for the excellence in her role.[2]

Mwaka 2019, Tamy aliteuliwa katika kinyang’anyiro cha msanii bora wa kike nyanda za Afrika ya Kusini karika tuzo za AFRIMA zilizofanyika nchini Ghana.[6]

Sanaa na Filamu hariri

Mwaka Filamu Uhusika Aina Marejeo.
2020 ‘’Gonarezhou Chipo Filamu

Marejeo hariri

  1. 1.0 1.1 1.2 "Tamy Moyo career". pindula. Iliwekwa mnamo 19 October 2020.  Check date values in: |accessdate= (help)
  2. 2.0 2.1 "NAMA opens Tammy Moyo acting career". herald.  Unknown parameter |access date= ignored (|access-date= suggested) (help)
  3. 3.0 3.1 3.2 "10 Things You Didn't Know About Teen Sensation Tammy Moyo". youthvillage. Iliwekwa mnamo 19 October 2020.  Check date values in: |accessdate= (help)
  4. comments, Blessing Masakadza • 2 October 2018 1:59 pm • 0. "ED's daughter in anti-poaching film". DailyNews Live. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-10-20. Iliwekwa mnamo 27 March 2019.  More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help); Check date values in: |accessdate= (help)
  5. "Tamy cherishes acting role". Daily News Zimbabwe. Iliwekwa mnamo 19 October 2020.  Check date values in: |accessdate= (help)
  6. "AFRIMA nomination a dream come true for Zim's Tammy Moyo". The Southern Times. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-10-27. Iliwekwa mnamo 19 October 2020.  More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help); Check date values in: |accessdate= (help)
  Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Tamy Moyo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.