Tandu-shamba
Spishi isiyotambuliwa ya Symphyla
Spishi isiyotambuliwa ya Symphyla
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia
Faila: Arthropoda
Nusufaila: Myriapoda
Ngeli: Symphyla
Ngazi za chini

Familia:

Tandu-shamba ni aina za arithropodi wadogo katika ngeli Symphyla ya nusufaila Myriapoda. Hata kama wanafanana na tandu wa kawaida, inaonekana kwamba wana mnasaba zaidi na majongoo lakini uchanganuzi wa ADN umetoa matokeo yanayopingana. Hawa ni wanyama wadogo wenye mm 2-30. Mwili wao ni mwororo na unapenyeka kwa nuru. Hawana macho na hutumia vipapasio ili kusikia njia. Huonekana katika udongo mpaka kina cha sm 50. Hula dutu ya viumbehai lakini spishi kadhaa zinaweza kuharibu mimea ya shambani.

Picha hariri

  Makala hii kuhusu "Tandu-shamba" inatumia neno (au maneno) ambalo si kawaida na matumizi yake ni jaribio la kutafsiri neno (au maneno) la asili garden centipede kutoka lugha ya Kiingereza. Neno (au maneno) la jaribio ni tandu-shamba.
Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao kwenye ukurasa wa majadiliano ya makala.

Kamusi za Kiswahili ama zinatofautiana kuhusu matumizi ya neno hili au hazieleweki au hazina neno kwa jambo linalojadiliwa.