Tenzi ni tungo ndefu za ushairi zinazoelezea juu ya mambo fulani na huwa na pande moja katika utenzi wake (yaani huwa na vina vya kati tu).

Tenzi huweza kuwa na mpangilio wa silabi zinazolingana katika kila mstari pia haufuati urari wa mizani katika mshororo wake.

Sifa za utenzi hariri

  1. Huwa na vina
  2. Huwa na mishororo minne
  3. Vile vile utenzi huwa na mizani nane
  4. Beti zake huwa nyingi ila hazizidi zile za utendi ambao wenyewe huwa na beti nyingi zenye usimulizi.mfano wa tenzi

Mifano ya tenzi hariri

1. Leo nataka binti,

Ukae juu ya kiti,

Ili uandike hati,

Ndogo ya waja.


Mimi kwako ni baba,

Hati hii ya huba,

Andikwa iwe haiba,

Asaa itakufaa.


Iwe kwako tiba,

Kwa shida za maswahiba,

Wasije wakaihiba,

Usije ukajutia.


2. Liyongo kitakamali,

Akabalighi rijali,

Akawa mtu wa kweli,

Na haiba kaongeya,

Twaitaka mbegu yake,

Nasi kwetu tuipeke,

Kwa furaha tumuweke,

Apate kutuzalia.

  Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Tenzi kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.