The Joplin Globe
The Joplin Globe ni gazeti la kuchapishwa kila siku kwa wiki katika eneo la Joplin, Missouri,Marekani. Linasambazwa katika makata 14 katika kusinimashariki mwa Missouri. Tangu mwaka wa 2002, imemilikiwa na shirika la Community Newspaper Holdings.
The Joplin Globe | |
---|---|
Jina la gazeti | The Joplin Globe |
Aina ya gazeti | Gazeti la kila siku |
Lilianzishwa | 1896 |
Nchi | Marekani |
Mwanzilishi | Thomas G. Barbee |
Mmiliki | Kampuni ya Magazeti ya Community (CNC) |
Mchapishaji | Dan Chiodo |
Makao Makuu ya kampuni | * 117 East Fourth Street * Joplin * Missouri 64801 |
Nakala zinazosambazwa | 30,558 kila siku |
Tovuti | http://www.joplinglobe.com |
Gazeti hili linaajiri wanahabari 45 katika chumba chake cha habari. Kaulimbiu yake ya masoko ni "Ni dunia yako. Sisi tunawasilisha tu." [1]
Habari ya Bonnie na Clyde
haririKatika mwaka wa 1933, The Joplin Globe ilipata habari muhimu sana ya kitaifa baada ya kupata kamera iliyoachwa nyuma na Bonnie na Clyde. Baada ya mapambano na polisi wa mtaa, walichapisha picha zilizotolewa kutoka filamu ya kamera hiyo. Picha hizi ni kama zile maarufu za Bonnie akimshika Clyde na kuigiza kuwa amemshikia Clyde bastola na za Bonnie akiwa akiwa ameshika bastola mkononi mmoja na sigara mdomoni mwake.
Mwanzilishi
haririThomas G. Barbee alizaliwa katika mwezi wa Oktoba 1870 katika Ritchey, katika kata la Newton, Missouri. Thomas alimwoa Laura (jina lake la pili halijulikani) aliyekuwa amezaliwa Januari 1874 katika Missouri. Barbee alimiliki Joplin Globe na akaanzisha kuchapisha gazeti la Joplin Tribune. Barbee alifariki tarehe 18 Oktoba 1924 katika Joplin, kata la Jasper, Missouri.
Marejeo
hariri- CNHI-CAN Circulation, figures for an undetermined date Ilihifadhiwa 12 Februari 2007 kwenye Wayback Machine.,.
- Joplin Globe FAQ Ilihifadhiwa 6 Oktoba 2008 kwenye Wayback Machine., .
- Court TV, CrimeLab website Ilihifadhiwa 22 Desemba 2008 kwenye Wayback Machine., ukurasa wa Bonnie na Clyde.