The Man-Eaters of Tsavo

The Man-eaters of Tsavo ni kitabu kilichoandikwa na John Henry Patterson mnamo mwaka wa 1907 na inaelezea maisha yake wakati alikuwa anajenga reli ya Uganda kupitia Kenya, kwa wengi inayojulikana sana kwa kurekodi hadithi ya jozi ya simba ambao aliwaua wakati alikuwa nchini Kenya, ambao pia walikuwa wanajulikana kama wala watu wa Tsavo. Kitabu hiki pia kina picha zilizochukuliwa na Patterson wakati huo ambazo zinajumuisha picha zilizopigwa wakati wa ujenzi wa reli; wafanyakazi; makabila ya Kenya; maonyesho maridadi na wanyamapori; na walaji binadamu ambao walikuwa simba.

The Man-eaters of Tsavo  
Faili:The Man-eaters of Tsavo book cover.jpg
Mwandishi (wa){{{mwandishi}}}
ISBNISBN:


Hadithi ya kitabu hiki imetumiwa katika filamu mara tatu: a monochrome, filamu ya Uingereza ya mwaka wa 1950, filamu ya mwaka wa 1952 ya 3-D ya iliyojulikana kama Bwana Devil l, na filamu ya mwaka wa 1996 toleo lililoitwa The Ghost and the Darkness ambapo Val Kilmer alicheza kama mhusika mkuu aliyekuwa mhandisi ambaye hakuwa na uoga wa kuwawinda simba wa Tsavo.


Kitabu hiki kinaelezea mashambulizi ya simba waliokuwa wanawala binadamu ambao walikuwa wajenzi wa Reli ya Uganda katika Tsavo, Kenya mwaka wa 1898 na jinsi simba hatimaye waliuwawa mwandishi wa kitabu hiki, Patterson. Hadithi hii ilikuwa ya ajabu kwani takriban watu 35 waliuawa na simba hao kwa muda wa chini ya mwaka mmoja kabla Patterson kuwaua (ingawa idadi hii inapingwa)


Kitabu hiki cha Patterson cha mwaka wa1907 chenyewe kinasema kwamba "kati yao (simba) hakuna chini ya Wahindi ishirini na nane ambao walinusurika kifo, pamoja na Waafrika ambao kwa bahati mbaya waliuwawa na ambao walikuwa wenyezji wa sehemu hiyo ". Idaidi hii ndogo ilithibitisha katika kitabu cha Dk Bruce Patterson cha The Lions of Tsavo: Exploring the Legacy of Africa's Notorious Man-Eaters (McGraw-Hill, 2004), ambayo iliandikwa jumba la maonyesho la Field Museum katika mji mkuu wa Chicago, ambapo simba hawa wameonyeshwa. Alionyesha kwamba idadi kubwa iliyotokana na simba ilitokana na jarida iliyoandikwa na Patterson mwaka wa 1925, iliyosema "simba hawa wawili waliwaua na kuwala wanadamu hawa kwa haraka, katika hali mbaya zaidi kwani idadi ya watu hawa ilikuwa mia moja na thelathini na tano iliyojumuisha Wahinidi naWaafrika ambao walikuwa wafanyikazi walioajiriwa katika ujenzi wa Reli ya Uganda. (The man-eating lions of Tsavo. Zoology: Jarida 7, Field Museum of Natural History, Chicago).


Kufuatia vifo vya simba hawa, kitabu kinaelezea ukamilifu wa reli na vilevile hadithi nyinginezo nyingi kuhusu wanyamapori wa humo nchini Kenya (pamoja na simba wengine), makabila ya Kenya, ugunduzi wa pango ya walaji wanadamu, na uwindaji mbalimbali wa vikundi.


Kitabu hiki pia kinajumuisha nyongeza ambayo inatoa ushauri watalii wote ambao wanaitembelwa Afrika Mashariki ya Uingereza (British East Africa kwa lugha ya Kiingereza).

Marejeo

hariri


Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu kitabu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu The Man-Eaters of Tsavo kama Mwandishi wake, hadithi au matoleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.