The Proposal ni filamu ya kuchekesha iliyotolewa 2009, iliyoongozwa na Anne Fletcher na kuigizwa na Sandra Bullock na Ryan Reynolds. Filamu hii ilitungwa na Pete Chiarelli.[2]

The Proposal
Imeongozwa na Anne Fletcher
Imetayarishwa na Todd Lieberman
David Hoberman
Alex Kurtzman
Roberto Orci
Kristin Burr
Imetungwa na Peter Chiarelli
Nyota Sandra Bullock,
Ryan Reynolds,
Malin Akerman
Mary Steenburgen
Craig T. Nelson
Betty White
Oscar Nuñez
Aasif Mandvi
Muziki na Aaron Zigman
Imehaririwa na Amanda Mackey Johnson
Cathy Sandrich
Imesambazwa na Touchstone Pictures
Imetolewa tar. Juni 1, 2009 (2009-06-01)
Ina muda wa dk. Dakika 108
Nchi Marekani
Lugha Kiingereza
Bajeti ya filamu $40 million[1]
Mapato yote ya filamu $314,658,031[1]

Hadithi hariri

Margaret Tate ni mhariri mkuu wa kampuni ya kuchapisha vitabu inayoitwa Ruick & Hunt Publishing. Wafanyikazi wake hawapendi uongozi wake. Baada ya kupata habari kuwa atarudishwa kwao nchini Canada, yeye anamlazimisha mtumishi wake, Andrew Paxton, amuowe ili apate kubaki nchini Marekani. Andrew anakubali kumuoa Margaret, lakini kwa masharti.

Wawili hawa wanaenda likizo kwa wazazi wa Andrew, kijijini Sitka, Alaska ili kuwadangaya familia yao kuwa wanaowana. Margaret anashikwa na bumbuwazi pindi anapogundua kuwa familia ya kina Andrew ni matajiri wanaomiliki biashara nyingi kijijini Sitka. Baada ya sherehe iliyoandaliwa nyumbani, Andrew anatangaza kuwa atamuowa Margaret.

Familia ya Andrew ilipokea habari hizo kwa furaha (isipokuwa babake Andrew) na wanapanga kuwa harusi ifanywe wiki hiyo hiyo. Harusi inapofanyika Margaret anaamua kuwa hawezi kuolewa na Andrew, na anatubia mbele ya kila mtu kuwa hiyo ilikuwa harusi ya uwongo. Margaret anaarifiwa kuwa ana saa 24 za kurudi Canada. Kwa sababu Margaret alikubali hatia aliyofanya, Andrew hakupelekwa jela. Margaret alirudi New York, na kufunganya vitu vyake. Andrew anakimbilia kumfuata na anampata Margaret ofisini anapomuambia kuwa anampenda mbele ya watu wote ofisini. Andrew anamposa Margaret, na wawili hawa na wachumba, na mara hii ni "kikwelikweli".

Waigizaji hariri

  • Sandra Bullock aliigiza kama Margaret Tate, mhariri mkuu wa kampuni ya kuchapisha vitabu.
  • Ryan Reynolds aliigiza kama Andrew Paxton, anayekubali kumuoa Margaret kwa sharti la kupandishwa cheo cha mhariri.
  • Mary Steenburgen anayeigiza kama Grace Paxton, mamake Andrew.
  • Craig T. Nelson aliigiza kama Joe Paxton, babake Andrew anayemtaka Andrew amiliki biashara alizonazo kijijini Sitka.
  • Betty White aliigiza kama Annie, nyanyake Andrew.

Kurekodi filamu hariri

Ingawa filamu hii ilichukuliwa kijijini Sitka, filamu hii ilirekodiwa katika eneo la Cape Ann mjini Massachusetts.

Muziki hariri

Ilitungwa na Aaron Zigman aliyerekodi nyimbo zake kwenye studio ya Hollywood Studio Symphony.[3]

Mafanikio hariri

Kwenye siku yake ya kwanza, filamu hii iliuza tikiti za milioni $12.7 kutoka kwa sinema 3,056, na kuwa namba 1 siku hiyo..[1][4] Filamu hii ilipata milioni $314 kote duniani na kuifanya filamu mojawapo ya Sandra Bullock iliyopata mafanikio iliyokusanya $163,958,031 kutoka nchi ya Marekani na Canada.

DVD hariri

The Proposal ilitolewa kwa DVD mnamo 13 Oktoba 2009.[5] Baada ya wiki mbili, iliuza nakala za DVD 3,314,840 na kupata $54,744,965.[6]

Tuzo hariri

Sandra Bullock alichaguliwa kwa tuzo la Golden Globe Award na akashinda tuzo la Teen Choice Award..[7] Pia, alishinda tuzo la People's Choice Award kwa kuwa muigizaji bora.

Marejeo hariri

  1. 1.0 1.1 1.2 "The Proposal (2009)". Box Office Mojo. Iliwekwa mnamo 2009-06-22. 
  2. The Proposal (2009)
  3. Dan Goldwasser. "Aaron Zigman scores The Proposal", ScoringSessions.com, 2009-05-06. Retrieved on 2009-05-06. 
  4. [1]
  5. Thorton, Michelle (17 Agosti 2009). ""The Proposal" On DVD October 13th". ReelEmpire.com. Iliwekwa mnamo 18 Agosti 2009. 
  6. [2].
  7. http://www.eonline.com/uberblog/b158058_complete_list_of_2010_golden_globe.html

Viungo vya nje hariri