Titanic (filamu 1997)
Titanic ni filamu ya kusikitisha na ya mapenzi inayohusu kuzama kwa meli ya Titanic. Filamu hii iliongozwa, ikaandikwa, ikatayarishwa na kuhaririwa na James Cameron mnamo 1997. Wahusika wake ni Leonardo DiCaprio kama Jack Dawson na Kate Winslet kama Rose DeWitt Bukater. Wawili hawa wenye maisha tofauti walipendana pindi walipokutana kwenye meli hii ambayo haikuwa na mwisho mwema.
Titanic | |
---|---|
Picha ya filamu ya Titanic | |
Aina | Mchezo wa mapenzi, Picha ya Kusikitisha |
Imetungwa na | James Cameron |
Imeongozwa | James Cameron |
Nchi inayotoka | Marekani |
Lugha | Kiingereza |
Utayarishaji | |
Watayarishaji wakuu |
James Cameron Jon Landau |
Muda | makisio ni dk. 194 |
Urushaji wa matangazo | |
Kituo | 20th Century Fox |
Inarushwa na | 19 Desemba 1997 |
Filamu hii ilikuwa itolewe mnamo 2 Julai 1997 lakini tarehe ikapelekwa mbele hadi 19 Desemba 1997.[1] Filamu hii ilipata mafanikio makubwa, kwa kushinda tuzo kumi na moja za Academy Awards.[2]
Kuhusu "Titanic"
haririMnamo 1912, Rose DeWitt Bukater (Kate Winslet) aliye na miaka kumi na saba anaingia kwenye meli mjini Southampton pamoja na mchumba wake aitwaye Caledon "Cal" Hockley (Billy Zane), tajiri mmoja aliye na miaka thelathini na mamake - Ruth DeWitt Bukater (Frances Fisher). Cal na Ruth wanasisitiza kuhusu sherehe ya uchumba wa Rose, kwani kuoana kwao kutatoa madeni yote ambayo familia ya DeWitt Bukater wanayo. Rose anataka kujiuwa kwa kujirusha baharini kutokamana na kulazimishwa kuolewa na mtu asiyempenda. Kabla hajajirusha, mchoraji mmoja aitwaye Jack Dawson (Leonardo DiCaprio) anamzuia. Papo hapo, Cal na rafiki zake wanaskia kelele alizopiga Rose na wakifika hapo wanadhania kuwa Jack alikuwa anataka kumbaka Rose. Rose anawaelezea kuwa Jack ameokoa maisha yake, kwani aliteleza na karibu aanguke pindi Jack alimshikilia. Hakusema ukweli kuwa alikuwa anataka kujiuwa. Jack na Rose wanaanza kuwa marafiki.
Jack anamchukua Rose kwenye sherehe iliyofanyika kwenye daraja la tatu. Cal alipopata habari, alimkataza Rose kuonana na Jack tena. Rose anakataa, na anamfuata Jack, akiona kuwa afadhali awe na Jack kuliko Cal. Jack na Rose wanaingia chumbani halafu Rose anamwambia Jack amchore akiwa uchi. Baada ya hapo, wawili hao wanafanya kitendo cha mapenzi. Papo hapo, meli hii inagonga jiwe laa barafu. Cal anaiona hiyo picha ya Rose, na kwa hasira, anatoa amri kwa askari wamshike na kumsingizia kuwa ameiba. Jack anafungwa pingu kwenye chuma ili asiweze kukimbia. Rose akatafuta panga na akavunja hizo pingu na kumfungua Jack. Meli inaanza kuvuja na kuzama.
Cal anamhimiza Rose apande dau ndogo itakayomuokoa. Rose anakubali lakini shingo upande. Mwishowe, alishuka kwenye dau na kurudi kwenye meli na kukumbatiana na mpenzi wake - Jack.Meli inapozama, Jack anatafuta kipande cha mbao watakacholalia ili wasizame. Kwa bahati mbaya, Jack anapata kipande kidogo cha kumtosheleza Rose pekee yake. Pindi waokoaji walivyokuja, Rose alimwamsha Jack lakini alikuwa amefariki kwa ajili ya maji yalivyokuwa baridi sana.
Wahusika Wakuu
hariri- Leonardo DiCaprio aliigiza kama Jack Dawson. Kwenye filamu hii, Jack ni mtu maskini hohe hahe. Anacheza mchezo wa kamari na kushinda tiketi ya kuingia kwenye meli ya Titanic. Anapendana na msichana wa kitajiri aitwaye Rose DeWitt.
- Kate Winslet aliigiza kama Rose DeWitt, ambaye ni msichana wa miaka kumi na saba aliyeposwa na jibaba tajiri la miaka takriban thelathini. Kate alimwacha tajiri na kupendana na Jack, aliye maskini hohehahe.
- Billy Zane aliigiza kama Caledon "Cal" Hockley ambaye ni mwanamume tajiri aliyetaka kumuoa Rose.
- Frances Fisher aliigiza kama Ruth DeWitt ambaye ni mamake Rose. Ruth ndiye aliyepanga uchumba wa Rose na Cal.
- Danny Nucci aliigiza kama FabrizioDe Rossi ambaye ni rafikiye Jack.
Wimbo wake
haririWimbo wake ulitungwa na James Horner. Wimbo huo wa "My Heart Will Go On" uliimbwa na Celine Dion.
Tuzo
hariri- Titanic ilishinda tuzo nne za Golden Globe za Best Motion Picture, Best Director, Best Original Score na Best Song.[3]
- Ilishinda tuzo 11 kutoka kwa Academy Awards.[4]
- Ilishinda tuzo tatu za Grammy Award: Record of the Year, Song of the Year na Best Song Written for a Motion Picture.[5]
- "My Heart Will Go On" ilishinda tuzo la Grammy Award ("Best Song Written Specifically for a Motion Picture or for Television").
- Hatimaye, Titanic ilishinda tuzo takriban 90 kote duniani.
Marejeo
hariri- ↑ Weinraub, Bernard. "Hollywood Braces for Likely Delay Of 'Titanic'", The New York Times, 1997-04-21.
- ↑ "Session Timeout - Academy Awards® Database - AMPAS". Awardsdatabase.oscars.org. Iliwekwa mnamo 2009-07-28.
- ↑ "Titanic sweeps Golden Globes", BBC, 1998-01-19. Retrieved on 2007-02-19.
- ↑ "Titanic". awardsdatabase.oscars.org. Iliwekwa mnamo 2010-01-19.
- ↑ "Grammy Award Winners". grammy.org. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-02-20. Iliwekwa mnamo 2010-01-06.
Viungo vya nje
hariri- Tovuti rasmi ya Titanic (filamu 1997)
- Titanic at the Internet Movie Database
- (Kiingereza) Titanic katika Allmovie
- Titanic katika Rotten Tomatoes
- Titanic katika Metacritic
- Titanic katika Sanduku la Ofisi la Mojo