Titanic
Titanic ilikuwa meli kutoka Uingereza iliyojengwa kati ya 1909 na 1912 huko Belfast. Wakati ule ilikuwa meli kubwa duniani pamoja na mwenzake "Olympic".
Titanic ilipotoka bandari ya Belfast kwa safari za kwanza za majaribio 2 Aprili 1912. | |
Habari za meli | |
---|---|
Wenye meli: | White Star Line |
Wajenzi: | Harland and Wolff shipyard, Belfasted |
Nahodha: | Edward John Smith |
Imeanzishwa: | 31 Machi 1909 |
Imepelekwa maji: | 31 Mei1 1911 |
Safari ya kwanza: | 10 Aprili 1912 |
Mwisho wa huduma: | Iligongana na siwa barafu tar. 13 Aprili 1912 ikazama baada ya masaa 3 tar. 15 Aprili 1912 |
Takwimu | |
Ukubwa wa meli: | 46,328 tani GT |
urefu: | 269 m |
Kina: | 10.5 m |
Mbio: | Kwa kawaida mnamo 26 km/h, hadi 44 km/h |
Mtindo wa kusogeza meli: | Rafadha mbili za mikono mitatu, rafadha moja ya kati yenye mikono minne |
Idadi ya abiria (safari ya kwanza): | 1912 - jumla 2,208
|
Ilipangwa kuzunguka kwenye Atlantiki kati ya Uingereza na Marekani.
Kwenye safari yake ya kwanza iligongana na siwa barafu tar. 14 Aprili 1912 mnamo saa sita kasorobo usiku ikazama baada ya masaa 2 na dakika 40 katika usiku wa tar. 15. Aprili.
Watu 2200 walikuwepo kwenye meli. Katika maji baridi takriban 1500 walikufa ni 700 waliookolewa na meli zilizokimbia kuokoa watu.
Ajali ya Titani ilionyesha kasoro nyingi katika sheria kuhusu ujenzi wa meli na vifaa kama idadi maboti madogo ya dharura na sheria zilibadilishwa baadaye.
1997 filamu juu ya kuzama kwa Titanic ilitolewa ikapata sifa nyingi.
Tazama pia
hariri
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Titanic kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |