Toleo Jipya la Hisa (Kenya)
Toleo Jipya la Hisa hutendeka wakati ambao kampuni inasajili hisa zake kwa mara ya kwanza katika Soko la Hisa la Nairobi. Kwa kusajili hisa zake katika soko, umma waweza kumiliki asilimia fulani ya kampuni hiyo kwa kununua hisa hizo.
Sababu ya Kusajili
haririSababu kuu ya makampuni kujisajili katika soko la hisa ni kuchangisha pesa ya kuendeleza matumizi yake mbalimbali. Wakati wa toleo jipya ya hisa za kampuni fulani, pesa zinazolipwa na umma ili kununua hisa hizi huenda kwa kampuni au wamiliki wa hisa hizo hapo awali.
Sabau za makampuni kuamua kusajili hisa zake kwenye soko ni kama vile:
- Kupata fedha ya kupanua biashara yao
- Uuzaji wa asilimia fulani ya kampuni kwa wamiliki wanaotaka kuondoka
Aina ya Hisa za Toleo Jipya
haririAina ya hisa za toleo jipya zaweza kuwa mawili:
Hisa Mpya
haririHii ni hisa mpya iliyotengenezwa ili isajilishwe kwenye soko. Wakati hisa hizi zinaponunuliwa:
- Rasilimali ya kampuni huongezeka
- Asilimia ya wamiliki wa kampuni hiyo hupunguka
- Rasilimali katika kampuni ya wamiliki hubaki vile vile
Hisa Mzee
haririHizi ni hisa zilizomilikiwa na wenyeji/mwenyeji wa kampuni. Wakati hisa hizi zinaponunuliwa:
- Rasilimali ya kampuni hubaki vile vile
- Asilimia ya wamiliki wa kampuni hiyo hupunguka
- Rasilimali katika kampuni ya wamiliki hupunguka
Taratibu ya Toleo Jipya ya Hisa
haririTaratibu ifwatayo hutumika ili kusajili kampuni katika soko la hisa kupitia toleo jipya la hisa:
- Kampuni inayotaka kujisajili kwenye soko huomba idhini kutoka kwa CMA (Capital Markets Authority)
- Baada ya kupata idhini, Benki ya Uwekezaji huchaguliwa kuongoza toleo hilo
- Taratibu ya ununuzaji kama vile nambari ya hisa mtu anaweza kununua hutangazwa kwa umma
- Walio na nia ya kununua hisa hizo katika umma huwasilisha maombi yao ya hisa kwa kujaza fomu an kuwapa mabroka wao. Hii huendelea hadi siku ya kufungwa kwa kupokea maombi ya hisa
- Maombi yaliyosajiliwa hupitiwa na kisha idadi ya hisa zilizoitishwa hutangazwa kwa umma. Kama idadi hii imepita hisa zilizosajiliwa na kampuni, waliojaza fomu za kununua hisa hawatapata hisa zote walizoomba.
- Hisa huanza kubadili katika soko baada ya kila mtu kupewa hisa alizoomba nao wale waliopewa hisa ndogo ya hile walioyoomba hurudishiwa fedha zao.
Angalia pia
haririViungo vya nje
hariri- Soko la Hisa la Nairobi Ilihifadhiwa 3 Januari 2010 kwenye Wayback Machine.
- "Capital Markets Authority"
- CDSC Kenya