Transformers (filamu)

Japani Marekani vyombo vya habari franchise

Transformers ni mfululizo wa filamu za kisayansi za hadithi za kutungwa.Michael Bay aliongoza filamu tano za kwanza: Transformers (2007), Revenge of the Fallen (2009), Dark of the Moon (2011) , Age of Extinction (2014), na The Last Knight (2017)[1][2], na amewahi kuwa mtayarishaji wa filamu zinazofuata[3]. Filamu ya sita ya Bumblebee, iliyoongozwa na Travis Knight na kutayarishwa na Bay, ilitolewa mnamo Desemba 21, 2018. Filamu ya saba, Rise of the Beasts, iliyoongozwa na Steven Caple Jr. na kutayarishwa na Bay, itatolewa mnamo Juni 9, 2023.

Logo ya Filamu zaTransformers

Mfululizo wa filamu hizi umesambazwa na kampuni ya Paramount Pictures, na DreamWorks zilifanya kazi kwenye filamu mbili za kwanza. Filamu za awali za Transfomers zilipata mapokezi mabaya kwa watazamaji , isipokuwa kwa Filamu ya Bumblebee, ambayo ilipata maoni mazuri kutoka kwa watazamaji. Ni katika nafasi ya filamu 14 zinazoingiza pato la juu zaidi, ikiwa na jumla ya dola bilioni 4.8; ikiwa Dark of the Moon na Age of Extinction zikiingiza zaidi ya dola bilioni 1 kila moja.

Marejeo

hariri
  1. "Producer Lorenzo Di Bonaventura Says 'Transformers 4' Coming For Summer 2014 | The Playlist". web.archive.org. 2012-04-19. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-04-19. Iliwekwa mnamo 2023-02-15.
  2. "Michael Bay To Direct 'Transformers 4,' Producer Confirms". MTV (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-03-29. Iliwekwa mnamo 2023-02-15.
  3. Adam B. Vary Updated February 14, 2012 at 07:38 PM EST. "'Transformers 4' lands Michael Bay as director". EW.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2023-02-15.{{cite web}}: CS1 maint: numeric names: authors list (link)