Hadithi
Hadithi (kutoka neno la Kiarabu) ni sehemu ya fasihi. Hasa kuna aina kuu mbili za hadithi:
- hadithi za matukio na wahusika wa kubuni,
- hadithi za matukio ya kubuni na wahusika wa kweli au kinyume chake.
Hadithi ni tungo za fasihi simulizi zitumiazo lugha ya nadharia.
Kwa maana ya pekee neno hili mara nyingi linataja hadithi za Mtume Muhammad ambazo zinahesabiwa kati ya misingi ya imani ya Uislamu.
Hadithi za kubuni
- Ngano za mazimwi: Wahusika wakuu huwa ni mazimwi ambao hupewa sifa zinazowatenga na binadamu wa kawaida.
- Ngano za mashujaa: Husimulia visa na vitendo na matukio ya kishujaa yanayohusiana na shujaa wa jamii fulani.
- Ngano za usuli: Hutoa asili au chanzo cha jambo.
- Hekaya: Hizi ni hadithi za kijanja... mhusika mmoja rafiki wa wengine hupitia njia ya hila na ujanja.
- Ghurufa: Wahusika huwa wanyama wanaowakilisha wanadamu wenye sifa za wanadamu hao.
- Ngano za kimafumbo: Huwa na mafumbo yenye maana nyingine ya ndani.
Vipera vya hadithi
Hadithi ina vipera vitano (5)
- Ngano
- Vigano
- Visasili
- Tarihi
- Soga.
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Hadithi kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |