Trilioni
Trilioni (kutoka Kiingereza "trillion") ni namba ambayo inamaanisha milioni mara elfu mara elfu moja, au milioni mara milioni na kuandikwa 1,000,000,000,000.
Inafuata 999,999,999,999 na kufuatwa na 1,000,000,000,001.
Inaweza kuandikwa pia kifupi 1 × 1012.
Matumizi tofauti
haririHesabu ya juu inafuata Kiingereza cha Marekani; kwa lugha nyingi za Ulaya trilioni ni 1018 na 1012 wanaita "bilioni".
Kimataifa kuna kawaida mbili tofauti kwa kutaja namba kuanzia milioni elfu moja au 109 [1]. Zinaitwa "skeli ndefu" na "skeli fupi":
- Kwenye skeli ndefu 1012 inaitwa bilioni na trilioni ni 1018. Wanatumia namba hivi: milioni 106, miliardi 109, bilioni 1012, biliardi 1015, trilioni 1018, triliardi 1021, quadrilioni 1024 na kadhalika. Skeli hii ni kawaida katika lugha nyingi za Ulaya pamoja na Kiingereza cha miaka iliyopita nchini Uingereza.
- Kwenye skeli fupi bilioni inaitwa 109 na trilioni ni 1012. Wanatumia namba hivi: milioni 106, bilioni 109, trilioni 1012, quadrilioni 1015, quintilioni 1018, sextilioni 1021, na kadhalika. Hii ni kawaida nchini Marekani na siku hizi pia Uingereza.
Mifumo yote miwili hutumia silabi za namba za Kilatini bi = 2, tri = 3, quadri = 4, quinti = 5, sexti = 6 na kadhalika ila hali halisi kwa namba kubwa sana ni kawaida kutumia umbo la tarakimu lama vile 106, 109, 1012 na kadhalika.
Inatokea mara nyingi ya kwamba skeli zote mbili zinachanganywa wakati wa kutafsiri vitabu au makala. Hapo ni afadhali kurudia namba kwa tarakimu.
Tazama pia
haririMarejeo
hariri- ↑ Kuhusu historia ya matumizi ya "milliard, billion", Trillion" katika lugha ya Kiingereza, tovuti ya linguistlist.org, iliangaliwa Januari 2018