Chuo Kikuu cha Tumaini
Chuo Kikuu cha Tumaini ni taasisi ya mafunzo ya juu nchini Tanzania iliyopo chini ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT).
Matawi ya Chuo Kikuu Tumaini
haririChuo kikuu Tumaini kina matawi manne:
- Chuo Kikuu cha Makumira (MUCo)
- Chuo Kikuu cha Tiba Kilimanjaro (KCMC)
- Chuo Kikuu Tumaini Iringa (IUCo)
- Chuo Kikuu Tumaini Dar es Salaam (TUDARCo)
Tawi la kwanza lilikuwa Chuo cha Theolojia Makumira huko Usa River, (Arusha) kilichoanzishwa mwaka 1947 kama mahali pa mafunzo kwa ajili ya wachungaji wa kanisa.
Tawi la pili liko Moshi mjini lajulikana hasa kama Kilimanjaro Christian Medical College (KCMC). Kilianzishwa mwaka 1971 kama hospitali ya Kikristo ya rufaa na ya kufundisha waganga.
Tawi la tatu lipo Iringa. Chuo kilianzishwa 1993 kwa jina la Chuo cha Kilutheri cha Iringa. Tangu 1995 masomo mbalimbali yaliongezwa: tangu 1995 biashara, tangu 1997 uandishi habari, tangu 1998 sheria, tangu 2001 ualimu. Vyeti vya kwanza vya bachelor vikatolewa 1998.
Tawi la nne lipo Dar es Salaam ambalo lilifunguliwa hivi karibuni.
Kuanzishwa kwa Chuo Kikuu 1996
haririMwaka 1996 vyuo vitatu vilivyokuwepo viliunganisha kuwa chuo kikuu cha kitaifa cha kilutheri. Azimio hili lilifuata sheria ya Tanzania na. 10 ya 1995 iliyoruhusu taasisi zisizo za kiserikali.
Utawala
haririMakao makuu yapo KCMC Moshi.
Askofu Mkuu wa KKKT huwa ni Chansella wa Chuo Kikuu. Chansella wa chuo hiki hivi sasa ni Dr. Samson Mushemba. Makamu wa chansella ni pofesa John F. Shao.
Viungo vya Nje
hariri- Tumaini University
- Tumaini University Dar es salaam College Archived 22 Agosti 2019 at the Wayback Machine.
- Iringa University College
- Kilimanjaro Christian Medical College Archived 1 Machi 2007 at the Wayback Machine.
- Makumira University College Archived 21 Aprili 2007 at the Wayback Machine.