Tume ya Chesapeake Bay

Tume ya Chesapeake Bay ni chombo cha ushauri kinachohusika na majimbo ya Maryland, Virginia na Pennsylvania kuhusu mazingira, uchumi na mambo ya jamii yanayohusiana na Chesapeak Bay. Tume inahusika kutia sahihi makubaliano yote yanayohusu hizo fukwe, na kuwashauri viongozi kwenye mambo yanayohusiana na fukwe hizo[1]. Hii tume ilianzishwa chini ya sheria ya mwaka 1980 na majimbo ya Maryland na Virginia. Pennsylvania alijiunga kwenye tume mwaka 1985[2].

Wanachama wa tume ni wabunge, makatibu wa baraza la mawaziri na wawakilishi wa wananchi. Mwaka 2022, mwenyekiti wa tume ni Sarah K. Elfreth, ambaye ni seneta wa Maryland[3]. Tume hukutana mara nne kwa mwaka, na ofisi za tume zipo Annapolis, Maryland; Richmond, Virginia; na Harrisburg, Pennsylvania.[4][5]

Marejeo hariri

  1. https://collections.unu.edu/eserv/UNU:2453/pdf9280811061_content.pdf
  2. "chesbay.us". www.chesbay.us (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-05-07. 
  3. "chesbay.us". www.chesbay.us (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-05-07. 
  4. "chesbay.us". www.chesbay.us (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-05-07. 
  5. "chesbay.us". www.chesbay.us (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-05-07.