Tuzo za Digital Impact Afrika
Tuzo za Digital Impact Afrika (DIAA), ni jukwaa linalokuza masuala ya kidijitali, masuala ya kifedha na usalama wa mitandao chini ya mada ya kuongeza gawio la digitali . Tuzo hizi zinalenga kutambua na kuthamini mashirika tofauti ambayo yanaongoza matumizi ya vyombo vya habari vya kidijitali.
Tuzo hizi zilianzishwa na HiPipo
Ustahiki wa tuzo
haririIli kuweza kushiriki, washiriki lazima wawe wamechangia kwa kiasi kikubwa katika nafasi za masuala ya kidigitali barani Afrika. Walioteuliwa wanaweza kuwa kutoka katika makampuni (SME), mashirika yasiyo ya faida, programu za kidijitali, miradi, mifumo na matangazo. Upeo wa mashirika wanaostahiki haujumuishi media.[1] Mradi huu unashughulikia nyanja kuu 3, ambazo ni masuala ya kidijiti, masuala ya kifedha na usalama wa mitandao. Umoja wa kimataifa wa mawasiliano (ITU), wakala maalumu wa Umoja wa Mataifa wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano- ICTs; iliorodhesha Tuzo za Digital Impact Afrika miongoni mwa miradi na matukio ya ICT ambayo yaliadhimisha Uorodheshaji wa ITU wa Maadhimisho ya miaka 150 tangu kuanzishwa kwa ITU.[2]