Habari (kutoka Kiarabu) ni mawasiliano ya maarifa kuhusu matukio ambayo huwasilishwa kwa watu kwa maneno ya kinywa, kwa maandishi kama vile magazeti, kwa matangazo ya masafa marefu kama vile redio au runinga, kwa intaneti n.k.

Neno hili linaweza kutumiwa pia katika sayansi kwa mawasiliano ya habari (kwa Kiingereza information, si news) kati ya seli za mwili, kwa mfano kati ya mkono na ubongo, kwa njia ya neva.

Historia ya kuripoti habari

Ukusanyaji wa habari ulipoanza, viwango vyake havikuwa vya hali ya juu vikilinganishwa na vya sasa. Ilibidi habari za kuchapishwa kuelezwa kupitia simu hadi kwenye kituo cha habari au kuletwa hapo na mwandishi, ambapo ilipigwa chapa na aidha kupelekwa kutumia huduma ya waya au kuhaririwa na kuwekwa pamoja na habari nyingine za aina moja kwa toleo maalumu.

Leo hii, neno "Mchipuko wa habari" limekuwa muhimu kwani huduma za matangazo na habari za amari (cable news) hutumia teknolojia ya satellite kuleta matukio ya sasa moja kwa moja majumbani mwa watumizi wa huduma hii. Matukio ambayo yalikuwa yanachukua masaa au siku kuwa maarifa ya kawaida katika miji au katika mataifa yanaletwa moja kwa moja kupitia redio, televisheni, simu kiini, na intaneti.

Magazeti

Miji mingi mikubwa ilikuwa na magazeti ya asubuhi na alasiri. Vyombo vya habari viliendelea kuwa na sehemu za kusambaza habari kuongezeka hadi kukaribia kupita kiasi. Hii ilisababisha magazeti za alasiri kufungwa zisipokuwa chache. Magazeti ya asubuhi yanapoteza mzunguko, kulingana na ripoti kutoka majarida yenyewe.

Kwa kawaida, habari zapaswa kuwa na taarifa tano za kawaida (nani, nini, lini, wapi, kwa nini, na pia jinsi gani?) katika tukio. Hakuna maswali ambayo yanapaswa kubaki. Magazeti kwa kawaida huandika habari nzito, kama zile zinazofungamana na uuaji, moto, vita na kadhalika. Ukitumia mfano wa piramidi uliogeuzwa habari muhimu ndizo zinazoanza. Wasomaji bizi wanaweza kusoma sana au kwa ufupi kulingana na shki yao. Stesheni za mitaa na mitandao yenye miundo lazima zichukue hadithi za habari na kuzivunja katika vipengele muhimu kutokana na vikwazo vya wakati. Chaneli za habari za amari kama Fox News, MSNBC, na CNN zina uwezo wa kuchukua faida ya hadithi, hadithi zenye umuhimu ndogo zikitolewa mhanga, na kutoa habari zinazochipuka kwa kina.

Usawa katika habari

Mashirika ya habari mara nyingi lengo lake hutarajiwa kuwa usawa; waandishi hudai kwamba wao hujaribu kufukua pande zote za suala bila upendeleo, ikilinganishwa na watangazaji au wachambuzi, ambao hutoa maoni au dhana ya binafsi. Hata hivyo, serikali kadhaa huweka baadhi ya vikwazo au huchunguza mashirika ya habari kama yana upendeleo. Kwa mfano, nchini Uingereza, mipaka huwekwa na wakala wa serikali, Ofcom (Office of Communications), ambayo ni ofisi ya Mawasiliano. Magazeti na vipindi vya matangazo ya habari nchini Marekani kwa ujumla yanatarajiwa kuepuka upendeleo isipokuwa makala yaliyodokezwa wazi. Serikali nyingi za chama kimoja zinaendesha mashirika ya habari, ambayo yanaweza kuwasilisha maoni ya serikali.

Hata katika hali ambazo usawa hutarajiwa, ni vigumu kupata usawa, na waandishi wa binafsi wa habari wanaweza kuwa na upendeleo wao, au kuangukia shinikizo la biashara au la siasa. Vivyo hivyo, usawa wa mashirika ya habari zinazomilikiwa na mashirika ya conglomerate zaweza kushukiwa katika mwanga wa asili ya motisha kwa vikundi vya habari kuripoti katika njia yenye nia ya kuendeleza maslahi ya kifedha ya conglomerate. Watu binafsi na mashirika ambayo ripoti ya habari imelengwa kwao wanaweza kutumia mbinu za usimamizi wa habari kujaribu kufanya hisia nzuri. Kwa sababu kila mtu ana mtazamo fulani, inatambulika kwamba hakuwezi kuwa na usawa katika kuripoti habari.

Karama ya habari

Karama ya habari hufafanuliwa kama masuala kuwa na manufaa ya kutosha kwa umma au hadhira maalumu kuhakikisha umakini wa watazamaji.

Watu wa kawaida si wa karama ya habari hadi wakutane ana kwa ana na hali isiyo ya kawaida au janga. Habari hii hugawanyisha umma katika makundi mawili; wale wachache ambao maisha yao ni ya karama ya habari na umati wa watu ambao huzaliwa, huishi na kufa bila vyombo vya habari kuwatambua hata kidogo. Daima habari hupitia masuala ambayo huvutia umakini wa watu na hutofautiana na maisha yao ya kawaida. Habari hii hutumiwa kwa uepushaji na kwa hiyo matukio ya kawaida si ya karama ya habari. Hata suala liwe upendo, uzazi, hali ya hewa, au uhalifu, ladha ya waandishi wa habari hukimbilia hali isiyo ya kawaida, ya ajabu.

Suala na karama ya habari ya hadithi inategemea na hadhira, kwani wao huamua ni nini linawafanya wawe au wasiwe na nia. Wakazi wakizidi, habari ya kuripotiwa ya kimataifa pia yaongezeka, kwani kuna maslahi mapana mbalimbali yanaohusika katika uteuzi wake.

Ni sehemu ya habari tu ambayo huonyesha jumla ya maendeleo duniani.

Vituo vya televisheni vya kutoa habari

Kituo Nchi Lugha Ilianzishwa Tovuti
KTN LEO Eacu Kiswahili 2017

[1] Archived 10 Desemba 2016 at the Wayback Machine.

Al Jazeera Kiarabu Live Stream http://oklivetv.com/al-jazeera-arabic-live/
ERITV Eritrea Kiarabu, Kiamhari, Kitigrinya 2017 http://www.eri.tv/
Tele-Tchad Tchad Kiarabu, Kihausa 2017 [2] Archived 2 Januari 2017 at the Wayback Machine.
A24 news channel Pan-African 2008 http://www.africawebtv.com/utv-ghana-online/ Africa Media
KBC Eacu Kiswahili 2016
Africa Black Tv Eacu Kiswahili, Kiarabu, Pijini(EN), Camfrancangle(FR), Kireno 2016

[3]

Rwanda TV Rwanda Kifaransa, Kiswahili, Kinyarwanda 2017 http://rba.co.rw/tv
Nyota TV Congo Zaire Kifaransa, Kiswahili 2016 http://www.nyota.net/category/videos/journal-tv/ Archived 21 Desemba 2016 at the Wayback Machine.
ZBC Zimbabwe Kiingereza, Kiswahili, Kishona 2016 http://www.zbc.co.zw/

Tazama pia

 
Simple English Wiktionary
Wikamusi ya Kiswahili ina maelezo na tafsiri ya maana ya neno:

Marejeo

  • Stephens, Mitchell. "The History of News - 3 Ed" Oxford University Press, New York, 2007.

Viungo vya nje