UNIX ni mfumo wa uendeshaji wa kompyuta. Ulianzishwa mwaka 1969 na Ken Thompson, Dennis Ritchie, Douglas McIlroy na wengine wengi huko Bell Labs. Walitumia lugha ya msimbo au ishara za ufupisho kuiandika.

Mwaka wa 1972, ishara za Unix zilirekebishwa tena na lugha mpya ya programu ya C.

Mfumo wa uendeshaji wa Unix ni mfumo wa watumiaji wengi na kufanya kazi kutumia kichakato zaidi ya kimoja. Hii inamaanisha inaweza kuendesha mipango kadhaa ya programu kwa wakati mmoja, kwa mtumiaji zaidi ya moja kwa wakati mmoja. Pia ina uwezo wa kufanya vizuri katika mtandao wa kompyuta.

Usalama wa kompyuta pia ni muhimu kwenye Unix, kwa sababu watu wengi wanaweza kuitumia hiyo, kwa kutumia kompyuta moja kwa moja au kwenye mtandao.