Uchaguzi wa Rais wa Marekani, 1912

Uchaguzi wa Rais wa Marekani, mwaka wa 1912 ulikuwa wa 32 katika historia ya Marekani. Ukafanywa Jumanne tarehe 5 Novemba. Upande wa "Democratic Party", Woodrow Wilson (pamoja na kaimu wake Thomas Marshall) aliwashinda mgombea wa "Republican Party" Rais William Howard Taft (pamoja na kaimu wake Nicholas Butler) na mgombea wa "Progressive Party", Rais wa zamani Theodore Roosevelt (pamoja na kaimu wake Hiram Johnson).

Matokeo

hariri

Wilson akapata kura 435, Roosevelt 88 na Taft nane tu. Ramani yaonyesha kura kwa kila jimbo.