Uchaguzi wa Rais wa Marekani, 1932

Uchaguzi wa Rais wa Marekani, mwaka wa 1932 ulikuwa wa 37 katika historia ya Marekani. Ukafanywa Jumanne tarehe 8 Novemba. Upande wa "Democratic Party", mgombea Franklin D. Roosevelt (pamoja na kaimu wake John Nance Garner) alimshinda mgombea wa "Republican Party" Rais Herbert Hoover (pamoja na kaimu wake Charles Curtis).

Matokeo hariri

Roosevelt akapata kura 472 na Hoover 59. Ramani yaonyesha kura kwa kila jimbo.