Katika hisabati, ugawanyaji (kwa Kiingereza: division) ni mojawapo kati ya vitendaji vinne vya hesabu (pamoja na ujumlishaji, utoaji na uzidishaji). Ugawanyaji ni kinyume cha uzidishaji. Alama ya ugawanyaji ni / au ÷

Alama ya mgawanyiko
Mfano wa 20/4 = matofaa 5.

Kwa usahihi, ugawanyaji ni tendo la kuhesabu idadi ya mara ambazo namba fulani inapatikana ndani ya namba nyingine. Kwa mfano, 20/4 = 5 kwa sababu tunaweza kuweka namba "4" mara tano ndani ya namba "20". Kugawanya ni kutoa namba fulani mara kadhaa kama vile kuzidisha ni kujumulisha namba fulani mara kadhaa.[1][2]

Marejeo

hariri
  1. Hisabati: Kitabu cha Mwanafunzi: Darasa la Tatu (tol. la 2). Taasisi ya Elimu Tanzania. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2024-04-18.
  2. Kinyondo, Abel. Mazoezi ya hisabati kwa kadi. University of Dar es Salaam Press.
  Makala hii kuhusu mambo ya hisabati bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ugawanyaji kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.